CHINA

Takriban Watu 40 wapoteza maisha baada ya kukumbwa na maporomoko ya udongo

Mvua kubwa zilizonyesha nchini China zimeharibu Makazi ya Watu
Mvua kubwa zilizonyesha nchini China zimeharibu Makazi ya Watu

Takriban watu 40 wamefukiwa na Maporomoko ya Udongo Kaskazini magharibi mwa China hii leo, Maafisa wameeleza, wakati huu mvua nzito zilizonyesha zimeharibu nyumba na madaraja.

Matangazo ya kibiashara

Maporomoko ya udongo mjini Zhongxing, jimboni Sichuan yalisababishwa na Mvua, Kikosi cha kuzima moto mjini Chengdu kimeeleza.
 

Maafisa mjini Zhongxing wamesema mpaka sasa familia 11 zimefukiwa na Zaidi ya wakazi 200 wameondolewa katika makazi yao,lakini Kikosi cha uaokoaji wanafanya jitihada kuwapata waliopotea.
 

Sehemu kubwa ya China imekuwa ikikumbwa na Mvua kubwa siku za hivi karibuni, yakiwemo maeneo kadhaa ya jimbo la Sichuan, ambapo Madaraja matatu yalivunjika tangu siku ya jumatatu.
 

Zaidi ya Waokoaji 2,700 walisambazwa kuwasaka watu 12 ambao hawajulikani walipo baada ya Daraja moja kuanguka jana.
 

Nyumba takriban 300 zimeharibiwa jimboni Sichuan na jimbo la jiran yunnan, Shirika la Habari la nchini humo, Xinhua limeripoti, na takriban Watu 36,800 wamehama makazi yao.
 

Mwezi Januari Watu 46 wengi wao Watoto walipoteza maisha kutokana na maporomoko ya udongo katika Jimbo la Yunnan, baada ya Wafanyakazi wa kikosi cha uokoaji zaidi ya 1,000 kuwasaka wale walionusurika kwenye tukio hilo.