CHINA

Idadi ya waliopoteza maisha kutokana na Maporomoko ya udongo nchini China yafikia 28

Mvua kubwa zilizonyesha nchini China zimeharibu Makazi ya Watu kusini magharibi mwa China
Mvua kubwa zilizonyesha nchini China zimeharibu Makazi ya Watu kusini magharibi mwa China

Watu 28 wamepoteza maisha na 66 hawajulikani walipo, maafisa nchini China wameripoti hii leo baada maporomoko ya Udongo kukumba Nyumba kuharibu Madaraja, Kusini magharibi mwa China.

Matangazo ya kibiashara

Mvua kubwa zilianza kunyesha siku ya Jumatatu na imeathiri Watu milioni 1.45 katika jimbo la Sichuan.
 

Maeneo kadhaa nchini China yamekumbwa na Mvua kubwa siku za hivi karibuni hasa katika maeneo ya milimani mvua zilizosababisha Maporomoko ya udongo.
 

Takriban Watu 2000 wamenasa kutokana na maporomoko hayo na wengine waliokolewa jana wakati huu ambapo Timu ya uokoaji ya dharura ikifanya jitihada za kuondoa udongo katika Barabara iendayo katika Vijiji 40 vilivyathiriwa na Maporomoko.
 

Wakazi wa Jimbo la Sichuan takriban 110,000 wameyaacha makazi yao kutokana na tufani ambayo imeleta madhara nchini humo.