CAMBODIA

Wapinzani wapinga matokeo ya uchaguzi nchini Cambodia

Reuters/Samrang Pring

Chama cha upinzani nchini Cambodia cha CNPR kimekataa kutambua matokeo ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita, matokeo hayo yalikipa ushindi mkubwa chama tawala cha CPP kambacho kimenyakua idadi kubwa ya viti.

Matangazo ya kibiashara

Upinzani nchini humo unasema kulikuwa na wizi mkubwa wa kura na wanataka uchunguzi ufanyike ili kubaini ni vipi chama cha CPP kilipata ushindi wa viti 68 kati ya 123 vilivyokuwa vinawaniwa.

Mbali na upinzani waangalizi wa kibinafsi waliokuwa wanachunguza uchaguzi huo wamesema kulikuwa na dosari nyingi katika zoezi hilo lote na uwezekano wa uchgauzi huo kutokuwa huru na haki ulikuwa mkubwa.

Kiongozi wa upinzani Sam Rainsy, ambaye alirejea nchini humo baada ya kuishi uhamishoni kwa kipindi kirefu ameishtumu serikali ya Waziri Mkuu Hun Sen ambaye amekuwa akiongoza nchi hiyo kwa miaka 28 kuendeleza unyanyasaji wa haki za binadamu na kudidimiza uhuru wa kisiasa nchini humo.

Waziri Mkuu Sen mwenye umri wa miaka 60 kabla ya uchaguzi huu alinukuliwa akisema hataondoka madarakani hadi atakapokuwa na umri wa miaka 74.