Korea kaskazini

Korea kaskazini na Kusini kurejea kwenye meza ya mazungumzo

Eneo la Viwanda la Kaesong
Eneo la Viwanda la Kaesong Photo: AFP

Korea kaskazini na korea kusini kwa pamoja zitafanya awamu ya saba ya mazungumzo siku ya jumatano juu ya kufunguliwa kwa eneo la kiviwanda la Kaesong.

Matangazo ya kibiashara

Awali Korea kaskazini ilifunga njia za kuelekea kwenye eneo la Kaesong, lililoko kilometa 10 ndani ya mpaka wa Korea kaskazini, na baadae kuondoa Wafanyakazi wake 53,000 ambao walikuwa wakifanya kazi na katika viwanda 123 vya Korea kusini vilivyo Kaesong.
 

Juma lililopita,Wakati Korea kusini ikitangaza kuwa itawalipa fidia ya kiasi cha dola za Marekani 250 wafanyabiashara walioathiriwa na kufungwa kwa eneo la kiviwanda la Kaesong, Korea kaskazini wakapendekeza kufanyika kwa mazungumzo mapya.
 

Korea kusini inatarajia kuanza mazoezi ya kijeshi sambamba na Marekani juma lijalo, mazoezi kama hayo yaliyofanyika awali ilikuwa sababu kwa Korea kaskazini kufunga eneo la viwanda la Kaesong.
 

Mazoezi ya Korea kusini na Marekani yanaelezwa na wachambuzi wa mambo kuwa yatasababisha kuwepo kwa vitisho na chokochoko kwa Korea Kaskazini