Korea kaskazini

Korea Kaskazini na Kusini zafikia muafaka juu ya mustakabali wa eneo la kiviwanda la Kaesong

Eneo la kiviwanda la Kaesong
Eneo la kiviwanda la Kaesong Photo: AFP

Korea kaskazini na kusini zimefikia makubaliano ya kufunguliwa tena kwa eneo la kiviwanda la Kaesong eneo lililofungwa na Pyongyang mwezi Aprili kutokana na tishio la mapigano kati ya nchi hizo.

Matangazo ya kibiashara

 

Makubaliano hayo yaliegemezwa katika maswala matano muhimu ambayo yamelazimu nchi hizo kufanya jitihada kurejesha eneo hilo ili lianze kufanya kazi haraka iwezekanavyo.
 

Kamati ya pamoja itaundwa kwa ajili ya kutathimini na kujadili namna ambayo nchi hizo zitalipa fidia kwa Walioathirika kwa kufungwa kwa Kaesong .
 

Kamati hiyo itasaidia kuondoa msuguano kati ya nchi hizo wakati huu ambapo Korea kusini ikitarajia kufanya mazoezi ya kijeshi Pamoja na marekani juma lijalo, mazoezi ambayo korea kaskazini imesema mazoezi ya kivita.
 

Pande hizo mbili zimeshakutana mara sita bila mazungumzo hayo kuzaa matunda juu ya mustakabali wa eneo la Kaesong lililofungwa na Korea Kaskazini mwezi Aprili baada ya kuwepo kwa mgawanyiko katika eneo hilo la Peninsula.
 

Kiongozi wa Ujumbe wa Korea kusini Kim Ki-Woong amesema kuwa awamu hii ya mazungumzo inaonesha kuwa suala linalowaweka mezani ni gumu kulitatua na kufikiwa kwa muafaka.
 

Shirikikisho linalowawakilisha wamiliki wa Makampuni 123 wa Korea Kusini ndani ya eneo la kiviwanda la Kaesong lilisema huu ni wakati mwafaka kuhakikisha kuwa mazungumzo hayo yanazaa matunda na kuanza kazi kwa Viwanda katika eneo hilo.
 

Korea Kaskazini ilipendekeza kuanza kwa mazungumzo ya awamu nyingine, saa kadhaa baada ya Serikali ya Korea kusini kutangaza kuwalipa fidia Wafanyabiashara waliathirika na kufingwa kwa Kaesong.