INDIA-AJALI YA TRENI

Watu 37 wapoteza maisha katika ajali ya treni iliotokea huko nchini India

Ajali ya Treni India
Ajali ya Treni India

Takriban mahujaji 37 ya madhehebu wa Hindu, wameuawa katika ajali ya treni nchini India katika jimbo la Bihar kwenye umbali wa kilometa 200 na mji mkuu wa jimbo la Patna wakati treni hiyo ilipo kwenye mwendo wa kasi na kugonga kundi la watu hao. Watu 35.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa shirika la reli Arun Malik ameliambia amesema kwamba, wananchi wenye hasira walivamia kituo cha treni cha Dharhara na kukiteketeza kwa moto pamoja na mabehewa ya mizigo.

Jumla ya mabehewa sita ya mizigo yameteketezwa kwa moto huku wafanyakazi wakitimka kuhofia maisha yao.

Kwa mujibu wa kiongozi mkuu wa baraza la kitaifa la shirika la reli, Arunendra Kumar, mahujaji hao walikuwa hawana habari yoyote kuhusu ujio wa treni, ambapo kuliko na orodha ya treni mbili ambazo zilizokuw azinafuatana na treni ya shirika la Rajya Rani Express ndiyo ilioruhisiwa kuondoka. Ajali hiyo ilitokea wakati watu waliposhuka kwenye treni ili kuvuka.

Mtandao wa reli nchini India unaosimamiwa na Serikali, hubeba watu milioni 18.5 kila siku na ni njia ya msingi ya usafiri wa umbali mrefu katika nchi hii kubwa ya watu bilioni 1.2, iambapo wengi hawana uwezo wa kusafiri kwa ndege.

Lakini idadi ni ya kushtusha kuhusu usalama: kila mwaka ajali mia tatu zinaorodheshwa, mara nyingi ikiwa ni ajali mbaya, zinazo tokana na migongano au kwa kuacha njia.

Kulingana na ripoti rasmi ya 2012, karibu watu 15,000 hufa kila mwaka tu kutokana na kuvuka barabara ya reli, takwimu ambazo serikali inazichukulia kama "mauaji."