Mahakama nchi China ya sikiliza kesi ya mwanasiasa maharufu nchini humo Bo Xilai kwa siku ya pili

Bo Xilai wakati wa kusikiliza kesi yake Agosti 22, 2013.
Bo Xilai wakati wa kusikiliza kesi yake Agosti 22, 2013. REUTERS/China Central Television

Mwanasiasa mahiri nchini China ambaye umaarufu wake umeshuka kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya ulaji wa rushwa na matumizi mabaya ya madaraka Bo Shilai amejitokeza na kumuita mkewe mwendawazimu. 

Matangazo ya kibiashara

Mwanasiasa Xilai alipanda kizimbani kwa siku ya pili hii leo kuendelea kusikiliza kesi yake iliyoanza jana lakini miongoni mwa ushahidi uliowakilishwa ni pamoja na video inayomuonesha mkewe Gu Kailai akithibitsha ushiriki wake kwenye ulaji wa rushwa.

Ushahidi huo wa Kailai uliowekwa bayana mahakamani hii leo umeonekana kumkera mno Xilai ambaye alijitokeza na kudhiriki kumuita mkewe huo mwendawazimu kwa sababu anaongea vizuri ambavyo havina ukweli wowote.

Video hiyo ya Kailai inaelezwa ilirekodiwa mwezi uliopita na kueleza waziwazi namna ambavyo Xilai alihusika kwenye ulaji wa rushwa na kukichafua pakubwa Chama Tawala cha Kikomunisti.

Xilai kwa upande wake anasema mkewe huyo huenda akawa amechanganyikiwa kutokana na kuhusishwa kwenye mauaji ya Mfanyabiashara wa Uingereza Neil Heywood kitu ambacho kinatajwa kumchafua pia mwanasiasa huyo.