YEMEN

Machafuko yaendelea kushuhudiwa kusini mwa Yemen kutokana na visima vya mafuta

Askari polisi wawili na raia m'moja wameuwawa leo jumatatu katika makabiliano ya ufyatulianaji risasi katika mji wa Daleh, kusini mwa Yemen, duru za usalama zimefahamisha.Makabiliano hayo yalianza wakati wanamgambo wa kusini walijaribu kuingia kwa nguvu ndani ya makao makuu ya mkoa wa Daleh, ili kupandisha bendera ya taifa la zamani la yemen kusini, wakati lilikua bado huru kabla ya mwaka 1990.

Matangazo ya kibiashara

Askari polisi 4 na raia 11, wakiwemo 4 ambao wenye silaha, wamejeruhiwa katika makabiliano hayo ya ufyatulianaji risasi.

Hata hivo, duru za kijeshi zimefahamisha kwamba kumetokea makabiliano ya ufyatulianaji risasi kati ya wanajeshi na watu wenye silaha ambao ni kutoka jamii moja mashariki ya Moukaila, makao makuu ya mkoa wa Hadramout (kusini mashariki) mwa Yemen.

Watu wenye silaha wameshambulia kituo cha wanajeshi karibu na visima vya mafuta katika mkoa wa Ghail Bayamine.

Akihojiwa na shirika la habari la AFP, m'moja wa wakuu wa jamii iliyojihusisha na vurugu hizo, Ahmad Bamaiche, amesema kua watu wake walitaka washirikane na wanajeshi, kwani wana haki ya kulinda mali ya visima hivyo, ambavyo vinapatikana katika mkoa huo.

Mikoa ya kusini mwa Yemen imekua ikikumbwa na machafuko ya mara kwa mara kutokana na madai ya mali asili.