Pata taarifa kuu
BANGLADESH

Polisi nchini Bangladesh yatawanya wandamanaji na watu wawili wamepoteza maisha

Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Watu wawili wamepoteza maisha katika msuguano wa polisi na waandamanaji katika mji wa Bacca nchini Bangladesh ambapo waandamanaji walikuwa wanamtaka kiongozi wa upinzani aliyezuiliwa na polisi kuhudhuria kwenye mkusanyiko wao.Maandamano hayo yalizuiliwa na Polisi nchini humo kwa kuhofia kutokea kwa umwagaji wa damu.

Matangazo ya kibiashara

Polisi nchini humo wametuamia nguvu kwa kuwasambaratisha waandamanaji ambao wanataka kurefushwa kwa tarehe ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Januari tano mwakani.

Polisi ililazimika kutimia risase za moto bada ya kushindwa kuwamudu waandamanaji hao, huku upande wao wakitumia bomu za kinenyeji katika kukabiliana na polisi.

Nur Alam Siddiqui Kiongozi wa polisi, amesema kwamba wametumia risase za moto kuwatawanya waandamanaji hao ambao pia wametumia bomu za kienyeji katika makabiliano hayo.

Waandamanji hao walilenga kuenea katika miji mbalimbali lakini pia katika makao makuu ya upinzani.

Katika kitongoji cha Rampura, polisi wamewasambaratisha waandamani zaidi ya mia mbili waliokuwa na bomu za kienyeji na kusababisha kifo cha mtu mmoja miongoni mwa waandamanaji huku polisi mmoja akiuawa katika kituo cha treni cha Kamalapur.

Polisi wa usalama, walifaulu kumzuia kiongozi wa upinzani Khaleda Zia kuondoka nyumbani kwake kujiunga na waandamanaji.

Zia ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa serikali nchini Bangladesh alitarajia kuwahutubia wafuasi wake baada ya maandamano ya kumtaka waziri mkuu Sheikh Kasina kujiuzulu na kuahirisha uchaguzi.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.