JAPON-Usalama

Mlipuko mkali walitikisa jimbo la Mie nchini Japan na kusababisha vifo

RFI

Watu watano wameuawa na wengine zaidi ya kumi wamejeruhiwa katika mlipuko uliyotokea ndani ya kiwanda kimoja, mjini kati Japan, ambacho kiliwahi kufungwa miaka mitatu illiyopita kutokana na kutoheshimisha sheria. Mlipuko huo umetokea ndani ya kiwanda kinachomilikiwa na kampuni ya Mitsubishi Materials, katika jimbo la Mie(katikati ya mji), wakati kulikua na shughuli ya kurekebisha mitambo inayotumiwa kwa kutengeneza vifaa kwa utumiaji wa madini aina ya silicium, ameelezea AFP, msemaji wa kampuni ya Mitsubishi.

Matangazo ya kibiashara

“ Watu watano wamefariki na wengine kumi na mbili wamejeruhiwa, wakiwemo tisa ambao walijeruhiwa vikali”, amesema afisa wa polisi katika jimbo la Mie.

Afisa huyo amebaini kwamba moto uliyosababishwa na mlipuko huo ulmezimwa.
Polisi haijaanzisha uchunguzi kwa kuhofia kua kunaweza kukatokea mlipuko mpya, lakini vifaa vyote vya kemikali, ambavyo vinaweza vikasababisha hatari vimeondolewa.

Televisheni za Japan zimeonyesha picha za waokoaji wakiwabeba kwenye vipoyo watu waliyojeruhiwa na moto.

“ Nilisikia mlipuko mkubwa, na muda mchache baadae, niliona moshi mweupe ukitokea kwenye kiwanda”, amesema mfanyakazi m'moja wa kiwanda jirani.

Kiwanda hicho kiliyowaka moto, kimekua kikitengeneza vifaa vinavyotumiwa kwa kutengeneza mitamb ya kupokea mionzi ya jua.

Hata hivo kampuni ya Mitsubishi Materials inawaajiri watu 22,000 duniani kote.