THAILAND-Uchaguzi

Maelfu ya Polisi watanda nchini Thailand kwa ajili ya kulinda usalama wakati wa uchaguzi unaotishiwa kuvurugwa na upinzani

Polisi nchini Thailand wakijihami kuzuia maandamano
Polisi nchini Thailand wakijihami kuzuia maandamano

Maelfu ya polisi nchini Thailand watasambazwa kwenye vituo vya kupigia kura siku ya Jumapili, kwenye uchaguzi unatajwa kuwa kipimo kwa demokrasia ya nchi hiyo wakati huu upinzani ukitishia kuvuruga zoezi la kupiga kura.

Matangazo ya kibiashara

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa uchaguzi wa siku ya jumapili unanafasi finyu sana ya kumaliza mzozo wa kisiasa unaoshuhudiwa nchini humo wala kumaliza utawala wa waziri mkuu Yingluck Shinawatra na badala yake huenda ukashuhudia kuendelea kusalia madarakani kwa familia ya Shinawatra.

Upinzani nchini humo hii leo umesisitiza kususia zoezi la uchaguzi uliopangwa kufanyika siku ya jumapili kwa kile inachodai kuwa umeharakishwa na unalenga kuendelea kulinda maslahi ya familia ya Shinawatra inyaotetewa na utawala wa kifalme nchini humo.

Mgomo wa upinzani pia umeungwa mkono hata na baadhi ya vyama vingine vidogo ambavyo havijawahi kushinda kwenye uchaguzi wowote nchini Thailand vikionya kuwa hautakuwa huru na haki.

Jeshi nchini humo tayari limetangaza makataa kwa waandamanaji mjini Bangkon na maeneo mengine ya nchi kujihusisha kwenye vurugu zozote zinazolenga kuharibu uchaguzi huo.