UKRAINE-URUSI-Diplomasia

Waangalizi wa OSCE waachiwa huru na waasi Mashariki mwa Ukraine

Axel Schneider katikati akiwa na waangalizi wa OSCE baada ya kuachiwa huru na waasi wa Ukraine tarehe 3 Mei
Axel Schneider katikati akiwa na waangalizi wa OSCE baada ya kuachiwa huru na waasi wa Ukraine tarehe 3 Mei REUTERS/Mathieu Radoube

Mkuu wa timu ya waangalizi wa Umoja wa Ulaya OSCE walioachiwa huru na waasi wanaounga mkono serikali ya Urusi mashariki mwa Ukraine jana Jumamosi wameelezea kupata ahueni kubwa baada ya tatizo ambalo limedumu kwa zaidi ya juma moja.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari nje ya mji wa Donetsk baada ya kuachiwa kanali Axel Shneider amesema kuwa ni furaha kwao na ahueni kubwa.

Waangalizi hao walikamatwa na waasi wanaounga mkono serikali ya Urusi mnamo Aprili 25 na kuwekwa katika mji wa Slavyansk, ambapo wakati mmoja wapiganaji hao waliwalazimisha watoe habari kwa waandishi chini ya ulinzi.

Kuachiwa kwa waangalizi hao ambako hakukutarajiwa ni habari njema kwa Ukraine , baada ya tukio la umwagaji damu siku ya Ijumaa ambapo zaidi ya watu 50 walipoteza maisha,wengi wao katika moto wa kutisha uliotokea kwenye mji wa Odessa.

Hata hivyo mgogoro wa kimataifa kuhusu Ukraine umeongezeka huku Urusi ikisema kuwa kwa sasa itakuwa haina maana kwa jamhuri hiyo ya zamani ya Soviet kuandaa uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika tarehe 25 mwezi Mei.