INDIA-Uchaguzi

India: chama tawala chakubali kushindwa

Wafuasi wa chama kikuu cha upinzani cha BJP kinachoongozwa na Narendra Modi wakati wa kampeni za uchaguzi..
Wafuasi wa chama kikuu cha upinzani cha BJP kinachoongozwa na Narendra Modi wakati wa kampeni za uchaguzi.. REUTERS/Amit Dave

Chama cha upinzani cha Bharatiya Janata (BJP) kinachoongozwa na Narendra Modi kiko katika njia nzuri ya kupata peke yake ushindi usiyokua na upinzani na kujinyakulia wingi wa viti katika bunge la nchini India.

Matangazo ya kibiashara

Chama cha BJP kimepata viti zaidi ya 272 vilivyokua vinahitajika ili kipate ushindi bungeni.

Chama hicho huenda kikapata viti kati ya 316 na 328 kwa jumla ya viti 543, kulingana na tathmini iliyotolewa na NDTN pamoja na CNN-IBN, ambayo inaambatana na matokeo ya mwanzo ya uchaguzi.

Chama tawala Congress Party, ambacho kiliongoza kwa muda wa miaka 10 nchini India kimekubali kushindwa kwenye uchaguzi mkuu wa wabunge, na kukipongeza chama cha Bharatiya Janata (BJP).

“Tunakubali kuwa tumeshindwa, tuko tayari kutawaliwa na upinzani”, msemaji wa chama tawala akiwa pia kiongozi wa chama hicho, Rajeev Shukla, mbele ya waandishi wa habari kwenye makao makuu ya chama tawala.

Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa kiongozi wa upinzani, Narendra Modi anaongoza na anaelekea kupata ushindi katika taifa hilo lenye wapiga kura wengi duniani.
Hata kabla ya kura kuanza kuhesabiwa, kura za maoni zilikuwa zimeonyesha kuwa chama cha upinzani cha Bharatiya Janata kitapata ushindi na kukiondoa chama cha Congress Party ambacho kimekuwa uongozini kwa miaka kumi sasa.

Mabango ya uchaguzi ya mgombea urais kwa tiketi ya chama kikuu cha upinzani nchini India BJP, Narendra Modi.
Mabango ya uchaguzi ya mgombea urais kwa tiketi ya chama kikuu cha upinzani nchini India BJP, Narendra Modi. REUTERS/Adnan Abidi

Kuoneakana kupata ushindi kwa upinzani, kumeimarsuha biashara katika soko la hisa jijini New Delhi.

Nchini india kura zinahesabiwa kieletroniki, na kati ya wapiga kura milioni 800 waliosajaliwa kupiga kura milioni 500 ndio waliojitokeza kupiga kura kwa kipindi cha mwezi uliopita.
Kufikia mwisho wa siku ya leo, mshindi anatarajiwa kufahamika na kuchukua nafasi ya Waziri Mkuu Manmohan Singh anayemaliza muda wake.