THAILAND-Mapinduzi ya kijeshi

Thailand: jeshi lachukua mamlaka

Mkuu wa majeshi ya Thailand, Prayuth Chan-ocha, ameonekana kwenye televisheni za Thailand akizunguukwa na maafisa wenzake wa kijeshi na kutoa tangazo la mapinduzi.
Mkuu wa majeshi ya Thailand, Prayuth Chan-ocha, ameonekana kwenye televisheni za Thailand akizunguukwa na maafisa wenzake wa kijeshi na kutoa tangazo la mapinduzi. capture d'écran TV thaïlandaise

Kiongozi wa jeshi la Thailand, jenerali Prayut Chan-O-Cha, ametangaza alhamisi wiki hii mapinduzi ya kijeshi nchini Thailand na kubaini kwamba Thailand kwa sasa iko nchi uongozi wa kijeshi.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi limetangaza pia hali ya hatari na kuchukua hatua ya kutotembea tangu saa kumi na mbili jioni hadi saa moja asubuhi, huku likifuta kwa muda katiba ya nchi.

Jeshi hilo limeamuru vyombo vya habari kurusha tu habari ihusuyo mapinduzi, na kuwataka waandamanaji kurejea makwao.

 Mapinduzi hayo yanakuja baada ya kuchuhudiwa mvutano kati ya wanasiasa uliyodumu miezi saba.

Kiongozi huyo wa majeshi amesema kwenye televisheni ya taifa kwamba jeshi limechukua uamzi huo ili lirejeshe hali ya utulivu nchini baada ya taifa hilo kukumbwa na mvutano wa kisiasa.

“ Ili hali ya utulivu irejeye nchini kote, jeshi limeamua kuchukua madaraka kuanzia Mei 22”, amesema Chan-O-Cha.

Jeshi lachukua mamlaka nchini Thailande, Mei 22 mwaka 2014.
Jeshi lachukua mamlaka nchini Thailande, Mei 22 mwaka 2014. Reuters

Awali jeshi lilifahamisha kwamba halijafanya mapinduzi, bali lilichukua hatua ya kuongeza idadi ya wanajeshi katika mikoa mbalimbali, na kupiga marufuku mikusanyiko ya watu, kwa lengo la kuimarisha usalama.
Jenerali Chan-O-Cha,amewataka raia kuwa watulivu, huku akiwatolea wito wafanyakazi kuendelea kuripoti kazini kama kawaida.

Tangazo hili la mapinduzi ya kijeshi litolewa baada ya kikao cha pili cha mazungumzo yaliyowashirikisha wadau wote wanaohusika na mgogoro ili kujaribu kupata suluhu.

Kwa mujibu wa mashahidi, viongozi wa waandamanaji kutoka makundi hasimu mawili walipelekwa kwa magari ya kijeshi kwenye eneo kuliko kuwa kukifanyika mkutano, kabla ya tangazo la mapinduzi kutolewa.

Thailand imeshakumbwa na hali ya mapinduzi ya kijeshi takriban 18 kwa kipindi cha miaka 80, na mapinduzi ya mwisho ni ya mwaka 2006 dhidi ya waziri mkuu Thaksin Shinawatra, ambaye yuko ukimbizini.