THAILAND-Mapinduzi ya kijeshi

Thailand: mkuu wa majeshi ajitangaza waziri mkuu

Mkuuu wa majeshi ya Thailand alie ongoza mapinduzi ya kijeshi, Prayuth Chan-ocha, ajitangaza waziri mkuu.
Mkuuu wa majeshi ya Thailand alie ongoza mapinduzi ya kijeshi, Prayuth Chan-ocha, ajitangaza waziri mkuu. AFP PHOTO / PORNCHAI KITTIWONGSAKUL

Siku moja baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini thailand, mkuu wa majeshi alieongoza mapinduzi hayo, Prayuth Chan-ocha, amejitangaza waziri mkuu. Waziri mkuu wa zamani Yingluck Shinawatra pamoja na mawaziri wengine wengi wameripoti kweye makao makuu ya baraza la kijeshi baada ya kuitishwa na kiongozi huyo wa majeshi.

Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa 120 wakiwemo viongozi wa vyama vya kiraia pamoja na waziri mkuu alieng'olewa madarakani, Niwatthamrong Boonsongpaisan, wameripoti kwenye makao makuu ya baraza la kijeshi, huku viongozxi 155 wakichukuliwa hatua ya kutoondoka nchini Thailand.

Pigo kubwa kwa aliekua waziri wa zamani wa Thailand,Yingluck Shinawatra kwa kuchukuliwa hatua ya kutosafiri nje ya nchi.
Pigo kubwa kwa aliekua waziri wa zamani wa Thailand,Yingluck Shinawatra kwa kuchukuliwa hatua ya kutosafiri nje ya nchi. REUTERS/Athit Perawongmetha

Yingluck ambae ni miongoni mwa viongozi hao waliyochukuliwa hatua ya kutosafiri nje ya nchi, hawezi kumkuta ndugu yake Thaskin Shinawatra, ambae yuko ukimbizini, tangu alipotimuliwa madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 2006, na baadae kuhukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kashfa ya ufisadi.

Jenerali Prayuth Chan-ocha, ambae aliongoza mapinduzi ya kijeshi, kwa sasa amejitangaza waziri mkuu wa Thailand, huku akibaini kwamba anashikilia wadhifa huo kwa muda kabla hajapatikana mtu mwengine atakaeushikilia.

Wanajeshi wameimarisha udhibiti wa mitandao, huku wakiyatahadhari mashirika yanayotoa huduma ya mitandao kuzuia baadhi ya picha na habari ambazo “zinaweza kuhatarisha usalama wa taifa”.

Wanajeshi wa Thailand waimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali, baada ya kutangazwa mapinduzi ya kijeshi, Mei 22 mwaka 2014..
Wanajeshi wa Thailand waimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali, baada ya kutangazwa mapinduzi ya kijeshi, Mei 22 mwaka 2014.. REUTERS/Athit Perawongmetha

Jeshi limechukua tangu jana alhamisi hatua ya kutotemebea usiku, kupiga marufu mikutano na mikusanyiko ya watu. Hata hivo vijana waliandama jana mbele ya eneo la ukumbusho wa demokrasia na kuupuuza hatua hio.