INDIA-Ajali

India: treni zagongana na kusababisha vifo vya watu

Ajali katika sekta ya reli zimekua sugu nchini India.
Ajali katika sekta ya reli zimekua sugu nchini India. AFP/Télévision indienne

Treni ya abiria imegingana na trni ya mizigo mapema jumatatu hii asubuhi kaskazini mwa India, na kusababisha vifo vya watu kumi, kiongozi mmoja wa shirika la reli ameelezea shirika la habari la AFP.

Matangazo ya kibiashara

Idadi hio ya watu waliyopoteza maisha katika ajali hio iliyotokea karibu na mji wa Khalilabad huenda ikaongezeka , kwani bado kuna watu ambao wamekwama ndani ya mabehewa, ameendelea kusema kiongozi huyo.

Mabehewa sita yameacha njia, na kwa sasa shughuli za uokozi ilikujaribu kuwaondoa watu waliokwama ndani ya mabehewa zinaendelea, wamebaini viongozi.

“Tunajaribu kujua idadi ya wahanga. Tunayo taarifa ya mabehewa sita ambayo yaliacha njia, baadya ya ajali hio na kusababisha watu kumi kufariki”, kiongozi wa shirika la reli nchini India ameelezea shirika la habari la AFP, ambae hakutaka jina lake litajwe.

Treni hio ya abiria ilikua inatokea katika eno la Hisar, mjini Haryana, ikielekea katika mji wa Godakhdham katika jimbo jirani la Uttar Pradesh. Treni hizo mbili ziligongana karibu na mji wa Khalilabad, kilomita 700 mashariki mwa mji mkuu wa India, New Delhi.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya India, watu 20 huenda wamefariki katika ajali hio.

Wakati huo huo, waziri mpya mteule, Narendra Modi, ambae anatarajiwa kuapishwa jumatatatu hii mchana, ametoa salaamu zake za rambi rambi kwa familia ziliyofiwa kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter.

Hata kama India inaongoza kwa reli, bado hali ya usalama katika sekta hio imekua tete.

Ripoti iliyotolewa na serikali mwaka wa 2012 inabaini kwamba watu 15.000 wanafariki kila mwaka nchini India katika ajali za treni.