Ukraine: watu 40 wauawa katika mji wa Donetsk
Imechapishwa:
Watu 40, wakiwemo wapiganaji 38 na raia wawili wameuawa jumanne hii katika mapigano kati ya jeshi na waasi wa Ukraine yalioanza jumatatu wiki hii katika jitihada za kujaribu kilia upande kudhibiti uanja wa ndege wa Donetsk katika eneo la mashariki, mkuu wa manispa ya jiji la Donetsk amethibitisha.
Viongozi wa Kiev wamethibitisha kwamba wameurejesha kwenye himaya ya utawala uwanja huo.
Wakati huo huo Urusi imetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano haraka iwezekanavyo katika mji wa Donetsk, mashariki mwa Ukraine.
“ Jukumu la kwanza na mshikamano wa viongozi wa
Kiev, kufuatia matokeo ya uchaguzi wa urais, ni kusitisha kutumia jeshi kwa kukandamiza raia pamoja na pande zote mbili kusitisha machafuko, amesema waziri wa mambo ya kigeni wa urusi”, Sergueï Lavrov.
Hato yakijiri waziri mkuu wa Ukraine Arseni Iatseniouk, ametupilia mbali uwezekano wa kuanzisha mazungumzo ya moja kwa moja na Urusi ili kujaribu kukomesha machafuko ambayo yanaendelea kuathiri taifa la Ukraine, bila hata hivo kuweko kwa wasuluhishi kutoka mataifa ya magharibi.
“Kwa sasa mazungu kati ya Urusi na Ukraine hayawezekani iwapo Marekani na Umoja wa Ulaya havitaashirikishwa” amesema Iatseniouk katika kikao cha baraza la mawaziri, huku akibaini kwamba wanahofia kudanganywa na Urusi iwapo wataketi pamoja kwenye meza ya mazungumzo.
Jumatatu wiki hii rais mpya wa Ukraine Poroncheko amethibitisha kwamba amekua na matumaini ya kukutanakwa mazungumzo na rais wa Urusi Vladimir Putin, na mkutano huo ungeliandaliwa katikamwezi ujao.