AFGHANISTAN-Siasa

Afghanistan : Abdullah : Lazima ufanyike uchunguzi kuhusu wizi kura

Abdullah, ambaye ni moja kati ya wagombea kiti cha urais nchini Afghanistan aomba uchunguzi ufanyike kuhusu wizi kura.
Abdullah, ambaye ni moja kati ya wagombea kiti cha urais nchini Afghanistan aomba uchunguzi ufanyike kuhusu wizi kura. REUTERS/Ahmad Masood

Abdulah Abdullah mgombea kiti cha urais nchini Afghanistan amesisitiza jana kuwa uchunguzi wa kina lazima ufanyike kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya awali ya uchaguzi wakati ambapo matokeo yakitarajiwa kutangazwa hii leo.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na vyombo vya habari jana jijini Kaboul, Abdullah Abdullah amesema wanachokiomba kwa sasa ni kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu uwepo wa udanganyifu wa kura kabla ya kutangazwa kwa matokeo yoyote ya Uchaguzi, lakini pia kutenganisha kura zilizo halali na zisizo kuwa halali

Abdullah Abdullah mgombea kiti cha urais nchini Afghanistani akidai kuwa uchaguzi uligubikwa na wizi.
Abdullah Abdullah mgombea kiti cha urais nchini Afghanistani akidai kuwa uchaguzi uligubikwa na wizi. REUTERS/Mohammad Ismail

Abdullah anatuhumu uwepo wa udanganyifu wa kura tangu pale ilipofanyika duru ya pili ya uchaguzi wa rais Juni 14 kwa kuongeza kura nyingi zaidi kwa faida ya mshindani wake Ashraf Ghani.

Matokeo ya kwanza ya duru ya pili ya uchaguzi ambayo awali yalitakiwa kutangazwa Julay 2 na tume huru ya Uchaguzi, yamepangwa kuwekwa bayana hii leo baada ya kufanyika kwa uchunguzi kwa baadhi ya vituo vya kupigia kura. Tume ya uchaguzi nchini humo ilikubali kufanya uchunguzi kwa takriban vituo 1930 dhidi ya vituo elf 23.

Hata hivyo Abdullah Abdullah amesema idadi hiyo ni ndogo mno ukilinganisha na ukubwa wa tukio lenyewe la wizi wa kura.

Ashraf Ghani Ahmadzai, mgombea kiti cha urais nchini Afghanistani.
Ashraf Ghani Ahmadzai, mgombea kiti cha urais nchini Afghanistani. Reuters/Omar Sobhani

Ombi hilo la uchunguzi zaidi kwa vituo vya kura huenda likasababisha kurefushwa tena kwa muda wa kutangazwa matokeo ya uchaguzi, jambo ambalo linapingwa na upande wa mgombea mwenza Ashraf Ghani.