AFGHANISTAN-Siasa-Usalama

Afghanistan : washindani wawili katika duru ya pili ya uchaguzi wajitangaza washindi

Washindani wawili, Ashraf Ghani (kushoto), et Abdullah Abdullah (kulia).
Washindani wawili, Ashraf Ghani (kushoto), et Abdullah Abdullah (kulia). AFP Photo/Wakil KOHSAR

Abdullah Abdullaah amejitangaza mshindi katika uchaguzi wa urais uliyofanyika nchini Afghanistan, na kutupilia mbali matokeo yanayoonesha mshindani wake Ashraf Ghani anaongoza, huku kukiwa na wasiwasi kwamba huenda mchakato wa uchaguzi ukakumbwa na vurugu, na uwezekano wa kutokea machafuko ya kijamii.

Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa Abdullah Abdullah  mjini Kaboul wakifurahia ushindi.
Wafuasi wa Abdullah Abdullah mjini Kaboul wakifurahia ushindi. Reuters/Omar Sobhani

“Bila shaka tumeshinda uchaguzi”, amesema Abdullah mbele ya maelfu ya wafuasi wake ambao walikua wamekusanyika katika mji mkuu wa Afghanistan, Kaboul.

Jumatatu hii jioni, tume huru ya uchaguzi imetangaza kwamba Shraf Ghani ana nafasi nzuri ya kuwa rais wa Afghanistan, baada ya kuongoza kwa kura dhidi ya mshindani wake Abdullah. Ghani kwa sasa anaongoza kwa asilimia 56,4 ya kura dhidi mshindani wake, Abdullah ambaye kwa sasa ana asilimia 43,5, kulingana na matokeo ya muda ya duru ya pili ya uchaguzi uliyofanyika Juni 14.

Mkuu wa tume huru ya uchaguzi Ahmad Yusuf Nuristani ameonya kwamba matokeo hayo ni ya muda, na haya maanishi mshindi wa uchaguzi. Amebaini kwamba inabaki hatua ya kupokea na kuchunguza mashitaka, na shughuli hio itaendeshwa na tume ya kuchunguza mashitaka (ECC), ameendelea kusema.

Timu ya Abdullah ambayo imekua ikilani utaratibu uliyokua ukitumiwa katika uchaguzi na kudai kuwa mshindani wake Ashraf Ghani alikua akipewa kura za wizi ili apate ushindi. Timu hio ilibaini kwamba tume ya uchaguzi ilikua na mpango wa kumpasisha Ashraf Ghani kuwa rais kinyume na uamzi wa wananchi waliyopiga kura. Kwa upande wake Ghani amesema ameshinda kwa mujibu wa sheria.

Abdullah alionekanakuwa atashinda duru ya pili ya uchaguzi, baada ya kupata asilimia 45 ya kura dhidi ya 31.6 katika duru ya kwanza ya uchaguzi na kuchukua nafasi ya mtangulizi wake Hamid Karzai alietawala taifa la Afghanistan tangu watalibani walipotimuliwa madarakani mwishoni mwa mwaka 2001.

Wafuasi wa Ghani wamekua wakisheherkea ushindi usiku kucha katika miji ya Kaboul na Kandahar.

Wahuasi wa Ashraf Ghani mjini Kaboul wakifurahia ushindi.
Wahuasi wa Ashraf Ghani mjini Kaboul wakifurahia ushindi. RFI/Nicolas Ropert

Baadhi ya waangalizi wa kimataifa wana hofu ya kuzuka machafuko ya kijami kati ya makabila ya Tadjik, kaskazini, ambao ni wafuasi wa Abdullah na Patchoune, kusini na mashariki, ambao ni wafuasi wa Ghani.

Hayo yanajiri wakati kikosi cha wanajeshi wa Jumuiya ya Mataifa ya kujihami ya NATO wanajiandaa kuondoka nchini Afghanistan mwishoni mwa mwaka huu.