AFGHANISTANI-Usalama

Afghanistan : Taliban yashambulia uwanja wa ndege wa Kaboul.

Askari polisi wa Afghanistani wakijipanga ili kukabiliana na shambulio la Taliban katka uwanja wa ndege mjini Kaboul, Julai 17.
Askari polisi wa Afghanistani wakijipanga ili kukabiliana na shambulio la Taliban katka uwanja wa ndege mjini Kaboul, Julai 17. REUTERS/Omar Sobhani

Wanamgambo wa kundi la Taliban wameshambulia mapema alhamisi asubuhi uwanja wa ndege wa Kaboul, mji mkuu wa Afghanistani. Kundi la Taliban limekiri kutekeleza shambulio hilo. Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan, kundi la waasi wamepenya na kuingia kwenye uwanja wa ndege na kuanza kufyatua hovyo risase na makombora, lakini waasi wote wameuawa.

Matangazo ya kibiashara

“Baadhi ya wapiganaji wetu wakiwa na silaha za kila aina wameendesha shambulio dhidi ya uwanja wa ndege wa Kaboul. Kwa mujibu wa taarifa zetu za awali, adui amepata pigo kubwa”, msemaji wa talibani Zabihullah Mujahid amesema katika tangazo liliyotolewa na kundi hilo mapema alhamisi hii asubuhi.

Waasi wamefyatua risase na kurusha makombora wakitumia silaha za rashasha, huku eneo hilo likizunguukwa na helikopta za kivita za kikosi cha Umoja wa Mataifa ya Magharibi ya Kujihami NATO nchini Afghanista Isaf) pamoja na zile za Afghanistan, huku moshi ukitanda eneo nzima la uwanja wa ndege. Viongozi wa Afghanistan wamesema hakuna hasara waliyoipata katika shambuliyo hilo.

Jeshi limejibu haraka shambulio hilo kabla halijachukua sura nyingine, na muda mchache baadaye mapigano yamesitishwa”, amesema msemaji wa polisi kitengo kinachopambana na uhalifu, Gul Agha Hashimi.

Kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wa Afghanistan amabaye hakutaka jina lake litajwe amesema safari za ndege zimesitishwa kwa muda kwenye uwanja wa ndege wa Kaboul. Mashambulizi yamekua sugu katika uwanja wa Kabul.

Julai 3, kulitokea shambulio la makombora 3 kwenye uwanja wa ndege wa Kaboula na kusababisha hasara, ambapo helikopta nyingi ziliharibiwa ikiwemo ya rais Hamid Karzaï.