JAPANI-URUSI

Japan yaichukulia Urusi vikwazo

Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe
Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe REUTERS/Edgar Su

Urusi imebaini kwamba uamzi uliyochukuliwa na Japan wa kuichuklia vikwazo siyo uamzi sahihi kwa nchi jirani kama Japan. Japan imesema ina orodha mpya ya majina ya viongozi na taasisi ambazo zinajihusisha na kuchochea vurugu nchini Ukraine.

Matangazo ya kibiashara

“Japan kutangaza vikwazo zaidi dhidi ya Urusi ni uamzi usiyo sahihi kama nchi jirani kutokana na tuhuma zisiyo na msingi ambazo zimepitwa na wakati kuhusu hali inayoendelea nchini Ukraine”, imesema wizara ya mambo ya nje ya Urusi katika tangazi iliyotoa.

Hapo jana jumatatu Japan ilitangaza kuwachukulia vikwazo baadhi ya viongozi na taasisi ambazo zimesababisha mdororo wa kiusalama na kujitenga kwa eneo la Crimea, na tukio la hivi karibuni la kudunguliwa kwa ndege ya Malaysia Airlines kwenye mpaka kati ya Urusi na Ukraine. Vikwazo hivyo vinahusiana na kutokubaliwa kwa viongozi hao kusafiri nchini Japan.

“Japan itaendelea kuomba Urusi kutumia uwezo wake kwa kushawishi waasi, mashariki mwa Ukraine, ili watowe ushiriki wao katika uchunguzi wa kimataifa unaoendelea kuhusu ajali ya ndege ya Malaysia Airlines iliyodunguliwa”, alitanga msemaji wa serikali ya Japan, Yoshihide Suga.

Moscow imebaini kwamba tuhuma hizo zimepitwa na wakati, kwani Urusi ndiyo ilikua nchi ya kwanza kutaka kufanyike uchunguzi wa kimataifa kufuatia ajali hiyo.

Tangazo hilo la Urusi limewataka viongozi wa Japan kuwa huru kwa kuendesha siasa za nchi, bila kufuata siasa za Marekani.