PALESTINA-ISRAELI-HAMAS-Usalama

Gaza : shule la UN lashambuliwa, watu zaidi ya 40 wauawa

raia wa palestina wakiwa katika mjo ya madarasa ya shule ya Umoja wa Mataifa UNRWA katika kijiji cha Jabaliya, liliyoshambuliwa usiku wa Julai 29 kuamkia 30 mwaka 2014..
raia wa palestina wakiwa katika mjo ya madarasa ya shule ya Umoja wa Mataifa UNRWA katika kijiji cha Jabaliya, liliyoshambuliwa usiku wa Julai 29 kuamkia 30 mwaka 2014.. REUTERS/Mohammed Salem

Takribani wapalestina 16 waliokua wamekimbilia katika shule ya Umoja wa Mataifa mjini Gaza wameuawa mapema jumatano asubuhi, baada ya jeshi la Israeli kushambulia shule hiyo, kulingana na taarifa ziliyotolewa na idara inayotoa huduma za uokozi.

Matangazo ya kibiashara

Makombora yaliyorushwa na vifaru vya jeshi la Israeli yameteketeza madarasa ya shule inayomilikiwa na tawi la Umoja wa Mataifa katika mji wa Gaza UNRWA, idara ya kutoa huduma za uokozi imethibitisha, huki ikitoa idadi ya vifo vya watu 16 tofauti na ya mwanzo ya vifo vya watu 20.

Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa katika mji wa Gaza, amethibitisha vifo vya watu 15.

Raia wengi wa kipalestina wameomba hifadhi katika shule zinazomolikiwa na tawi la Umoja wa Mataifa katika mji wa Gaza, hususan katika kijiji cha Jabaliya, baada ya jeshi la Israeli kuwataka kuondoka katika kijiji hicho, likionya kwamba huenda kikashambuliwa.

Raia wa Gaza wakikimbilia katika shule za Umoja wa Mataifa kufuatia mashambulizi ya anga ya jeshi la Israeli.
Raia wa Gaza wakikimbilia katika shule za Umoja wa Mataifa kufuatia mashambulizi ya anga ya jeshi la Israeli. REUTERS/Finbarr O'Reilly

Takribani wapalestina 180.000 wameyahama makaazi yao kufuatia mashambulizi ya jeshi la Israeli, na kukimbilia katika shule 83 zinazomilikiwa na tawi la Umoja wa Mataifa UNRWA. Raia hao kwa sasa wanaishi katika mazingiria magumu.

Idadi kubwa ya shule hizo zimeshambuliwa kwa mabomu. Julai 24. jeshi la Israeli lilirusha bomu katika shule mojawapo ya shule zinazomilikiwa na UNRWA katika kijiji cha Bait Il Hanoun, na kuua wapalestina 15. Jeshi la Israeli lilikanusha kuhusika na shambulio hilo.

Israeli inalinyooshea kidole kundi la Hamas kuhusika na vifo vya raia wa Palestina, ikiwatuhumu kutumia raia kama ngao.

Siku moja kabla UNRWA ililani tabia ya Hamas ya kutumia moja ya shule zake kwa kuficha silaha na zana nyingine za kijeshi, huku ikibaini kwamba shule hiyo iliyokua ikitumiwa na Hamas, siyo ya Jabaliya iliyoshambuliwa usiku wa jumanne kuamkia jumatano wiki hii.

“Jana jumapili tumesema shule moja inayotumiwa na Hamas kwa kuficha silaha, iliyoko katikati ya mji wa Gaza, siyo shule ya Jabaliya iliyo kaskazini mashariki”, msemaji wa UNRWA, Chris Gunner, ameambia shirika la habari la Ufaransa AFP.

Kwa sasa idadi ya vifo katika ukanda wa Gaza imefikia 1500.