CAMBODIA-Sheria

Cambodia: hukumu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya viongozi wa wawili wa utawala wa Khmer Rouge

Hukumu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya viongozi wa wili wa utawala wa Khmer Rouge, yapokelea kwa furaha na familia za wahanga.
Hukumu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya viongozi wa wili wa utawala wa Khmer Rouge, yapokelea kwa furaha na familia za wahanga. REUTERS/Damir Sagolj

Mahakama maalumu nchini Cambodia inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, imetoa hukumu alhamisi wiki hii ya kifungo cha maisha jela dhidi ya watuhumiwa wawili waliongoza wakati wa utawala wa Khmer Rouge. 

Matangazo ya kibiashara

Hukumu hii ilikua inasubiriwa kwa hamu na wananchi wa taifa hilo na dunia kwa ujumla, na ni hukumu ya kwanza kutolewa dhidi ya waliokuwa viongozi wa utawala wa Khmer Rouge ambao walishtakiwa kwa makosa ya kivita.

Mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo, alitaka kutolewa kwa adhabu ya kifungo cha maisha kwa Nuon Chea mwenye umri wa miaka 88 na aliyekuwa mtawala wa wakati huo, pamoja na Khieu Samphan mwenye umri wa miaka 83, wakiwa ni viongozi wawili pekee waliohai na waliohudumu wakati huo.

Moja ya sehemu kulikozikwa watu waliouawa wakati wa utawala wa Khmers rouges.
Moja ya sehemu kulikozikwa watu waliouawa wakati wa utawala wa Khmers rouges. (Photo : S. Malibeaux / RFI)

Watuhumiwa hawa wanadaiwa kuamrisha mauaji ya zaidi ya raia milioni mbili wa Cambodia kati ya mwaka 1975 na mwaka 1979.

Hukumu hiyo imerushwa moja kwa moja na vyombo vya habari nchi nzima huku zaidi ya raia 900 wa Cambodia wakihudhuria mahakamani wakati wa usomwaji wa hukumu hiyo.

 Hata hivo, viongozi hao wa utawala wa Khmer Rouge watakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo alhamisi wiiki hii, wamesema mawakili wao.

“Tutakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo. Mteja wangu amefanyiwa unyonge”, amesema Son Arun, mwanasheria wa Nuon Chea , huku akibaini kwamba hukumu hiyo dhidi ya mteja wake ni kubwa mno. Naye Kong Sam, mwanasheria wa Khieu Samphan, amesema hakubaliani na hukumu hiyo, na ameamua kukata rufaa.