Iraq-VATICAN-mapigano

Iraq: wanamgambo wa kislamu wauteka mji wa Qaroqash

Wapiganaji wa makundi ya wanamgambo wa kislamu wanaoshikilia maeneo kadhaa kaskazini magharibi mwa Iraq wanaendelea kuteka maeneo mengine yaliyokuwa kwenye himaya ya jeshi la serikali ya Iraq mkiwemo mji wa Qaroqash unaokaliwa na wakisto.

Wapiganaji wa kikurdi wakati wa maqpigano dhidi ya wapiganaji wa makundi ya kislamu nchini Iraq.
Wapiganaji wa kikurdi wakati wa maqpigano dhidi ya wapiganaji wa makundi ya kislamu nchini Iraq. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Mamia kwa maelfu ya raia wameyakimbi makaazi yao kwa kuhofiya usalama wao baada ya miji ya Qaraqosh, Tal Kayf, Bartella, Makhmour, Al Kouair na Karamlesh kutekwa na wanamgambo wa kislamu.

“Raia wa miji ya Qaraqosh, Tal Kayf, Bartella na Karamlesh wameyahama makaazi yao baada ya miji hiyo kutekwa na wanamgambo wa kislamu wanaoshikilia maeneo ya magharibi mwa Iraq”, askofu Joseph Thomas wa Kirkouk amelithibitishia shirika la habari la Ufaransa AFP.

“Hili ni janga, hali ya kusikitisha. Tuna omba Baraza la Umoja wa Mataifa kuingilia kati haraka iwezekanavyo. Raia wengi wamefukuzwa katika makaazi yao, wakati huu tunaongea, hatujui hali halisi inayojiri katika mji huo wa Qaraqosh”, ameendelea kusema askofu Thoma.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Pope Francis ameitaka jumuiya ya kimataifa kuigilia kati ili kulinda usalama wa raia wa Qaraqosh.

Miji yote hio imetekwa usiku wa jumatano kuamkia alhamisi na wapiganaji wa kundi linaloongozwa na Abou Bakr Al-Baghdadi. Kwa mujibu wa mashuhuda, maelfu ya raia wameondka katika miji hiyo kabla ya kutekwa na wapiganaji hao.

Qaraqosh ni mji mkubwa wenye wakristu wengi nchini Iraq. Wanajeshi wa kikurdi waliondoka katika mji huo baada ya kutimuliwa na waasi hao wa kislamu.