URUSI-UKRAINE-Msaada

Urusi : Ukraine yainyooshea kidole Moscow

Kauli ya Urusi imeambatana na vitendo, baada ya kuahidi kutoa msaada wa kibinadamu kwa raia wa Ukraine. Takribani malori 280 yameondoka mapema jumanne asubuhi wiki hii katika jimbo la Moscow yakielekea nchini Ukraine. Hali ambayo imetia hofu jumuiya ya kimataifa na serikali ya kiev, ambayo imesema ni mbinu za Urusi za kutaka kuteka Ukraine kupitia msaada wa kibinadamu.

Msafara wa magari 280 ya Urusi yanayobeba msaada wa kibinadamu yakielekea nchini Ukraine.
Msafara wa magari 280 ya Urusi yanayobeba msaada wa kibinadamu yakielekea nchini Ukraine. REUTERS/Reuters TV
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Ukraine imebaini kwamba haitokubali msafara huo wa magari ya Urusi uingiye nchini Ukraine.

Kwa mujibu wa utawala wa jimbo la Moscow, serikali ya Ukraine kamwe haitokubali malori 280 yanayobeba tani 2000 ya vifaa na chakula yaingiye kwenye aridhi yake.
Ikulu ya Kiev imesema iwapo malori hayo ya Urusi yatavuka mpaka na kuingia nchini Ukraine, itakua ni kitendo cha uchokozi.

Kwa mujibu wa Valery Chaly, msaada huo utaweza kuruhusiwa kuingia nchini Ukraine iwapo utakabidhiwa shirika la msalaba mwekundu, bila hata hivo kutumia magari hayo ya Urusi. Valery Chaly amebaini kwamba shirika la Msalaba mwekundi litapokea msaada huo wa Urusi kwa idhini ya serikali ya Ukraine. Urusi bado haijatoa msimamo wake kuhusu kauli hiyo ya serikali ya Ukraine.

Hatuna haja kwa viongozi wa Ukraine kupokea msafara huo wa Urusi, ambao huenda unashindikizwa na wanajeshi wa Urusi aidha maofisa wa wizara ya hali ya dharura, amesema mshauri wa rais wa Ukraine, Petro Porochenko. Msemaji wa jeshi la Ukraine, idhini ya kuingia kwenye aridhi ya Ukraine inaendana na mahitaji yanayopangwa na shirika la msalaba mwekundu kwa kila mkoa katika wiki moja. Shirika la msalaba mwekundu limejizuia kutoa taarifa yoyote.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Ukraine, Danylo Lubkivsky, amesema anatiwa hofu na Urusi ambayo inaweza kutumia msaada huo kwa kuingilia kijeshi taifa la Ukraine. Hata mataifa ya magharibi yamesema kutiwa hofu na msaada huo wa Urusi. Kwa upande wake rais wa Ufaransa François Hollande amezungumza kwa njia ya simu na mwenziye wa Urusi Vladimir Putine, akimueleza kutiwa hofu na uamzi wa Urusi wa kuingiza magari yake nchini Ukraine bila kushirikisha mataifa mengine.