SYRIA-ISIL-Mapigano-Usalama

Syria: wapiganaji wa Isil wanaendelea kupata ushindi dhidi ya waasi

Wapiganaji wa ISIL wakiendelea kuteka maeneo yaliyokua yakishikiliwa na waasi nchini Syria.
Wapiganaji wa ISIL wakiendelea kuteka maeneo yaliyokua yakishikiliwa na waasi nchini Syria. REUTERS/Stringer

Mapigano yanaendelea kushuhudiwa nchini Syria kati ya waasi wa Syria na wapiganaji wa makundi ya wanamgambo wa kislamu wanaoshikilia baadhi ya maeneo ya Syria na Iraq.

Matangazo ya kibiashara

Duru za kuaminika zinafahamisha kwamba wapiganaji wa makundi hayo wanaendelea kupata ushindi katika uwanja wa vita dhidi ya waasi hao wa Syria. Taarifa hiyo imethibitishwa na televisheni France 24.

Wapiganaji hao wa Isil wameendesha mashambulizi jumatano wiki hii dhidi ya ngome za waasi na kuyateka baadhi ya maeneo yanayoshikiliwa na waasi. Mapigano hayo yamesababisha vifo vya watu 52, shirika la haki za binadamu nchini Syria(OSDH) limethibitisha.

Wapiganaji wa kislamu wa ISIL wakiendelea na mapigano nchini Iraq.
Wapiganaji wa kislamu wa ISIL wakiendelea na mapigano nchini Iraq. REUTERS/Stringer

“Kundi la wapiganaji wa kislamu Isil wameteka maeneo 8 kwa muda wa saa 24 kaskazini mwa mwa mji wa Allepo, jirani na mpka wa Uturuki.Vijiji vya Arshaf na Dabeq ni miongoni mwa maeneo yaliyotekwa”, shirika hilo limesema.

Takribani waasi 40 na wapiganaji 12 wa Isil wameuawa katika mapigano hayo, kwa mujibu wa takwimu mpya ya OSDH, tofauti na taarifa za awali ziliyotaja watu 39 kuwa ndio waliuawa katika mapigano kati ya waasi na wapiganaji wa Isil.
Kwa mujibu wa OSDH, wapiganaji wa Isil wamewashikilia mahabusu waasi 50.

Rais wa Ufaransa, François Hollande,akiapa kusaidia wakurdi kupambana na wapiganaji wa kslamu nchini Iraq.
Rais wa Ufaransa, François Hollande,akiapa kusaidia wakurdi kupambana na wapiganaji wa kslamu nchini Iraq. REUTERS/Benoit Tessier

Hayo ya kijiri rais wa Ufaransa Francois Hollande jumatano wiki hii alitangaza kuwa taifa lake liko tayari kuwahami wapiganaji Wa kikurdi nchini Iraq ili wakabiliane na wapiganaji wa ISIL ambao wanaendelea na mapigano kaskazini mwa nchi hiyo.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari vya Ufaransa, rais Hollande amepata ruhusa kutoka kwa mamlaka nchini Iraq kuendelea mbele na mpango huo mahsusi wa kulidhibiti eneo lililotangazwa na wapiganaji hao kuwa la kisilamu.

Wapiganaji wa kikurdi wamekuwa wakikabiliana na wapiganaji wa wanamgambo wa Islamic State ambao wameunda himaya yao kaskazini mwa Iraq pamoja na sehemu za Syria.