THAILAND-Mapinduzi ya kijeshi-Siasa

Thailand: kiongozi wa mapinduzi achaguliwa kuwa waziri mkuu

Afisa wa ngazi ya juu katika jeshi laThailand, aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi, jenerali Prayuth Chan-ocha, amechaguliwa na Bunge kuwa waziri mkuu wa serikali ya mpito, Uchaguzi huo si mshangao, kwani jeshi linajaribu kuingilia mchakato wa mabadiliko katika taasisi zote za nchi kabla ya uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka ujao.

Waziri mkuu mpya wa Thailand, jenerali Prayuth Chan-ocha, Agosti 21 mwaka 2014, katika mkoa wa Chomburi.
Waziri mkuu mpya wa Thailand, jenerali Prayuth Chan-ocha, Agosti 21 mwaka 2014, katika mkoa wa Chomburi. REUTERS/Chaiwat Subprasom
Matangazo ya kibiashara

Jenerali Prayuth Chan-ocha, amechaguliwa na wabunge wote wa bunge la Thailand, kwani wabunge hao waliteuliwa na jershi baada ya mapinduzi. Hata hivo spika wa Bunge na makamu wake wawili hawakutoa msimamo wao kama zinavyoeleza taratibu za bunge la Thailand.

Mchakato huo unaonesha wazi kwamba jeshi limeanza mkakati wa kuingilia mabadiliko ya shughuli za siasa ya taifa hilo, na hali hiyo inaashiria kwamba katiba ijayo ya nchi itaminya mfumo mzima wa kidemokrasia, ambapo jeshi linadai kwamba itachangiya kukuza demokrasia.

Uteuzi wa mawaziri mbalimbali wa serikali ya mpito utatangazwa hivi karibuni, lakini imeshajulikana kwamba serikali hiyo itaundwa na idadi kubwa ya wanajeshi. Hali hiyo inakumbusha mfumo wa kiimla wa miaka 1960, ambapo wanajeshi ndiyo walikua na mamlaka ya nchi.