AFGHANISTANI-NATO-Usalaama-Siasa

Afghanistan: wazairi wa ulinzi anatazamiwa kushjriki mkutano wa Nato

Rais wa Afghanistan anaeondoka madarakani, Hamid Karzai.
Rais wa Afghanistan anaeondoka madarakani, Hamid Karzai. REUTERS/Mohammad Ismail

Huenda waziri wa Ulinzi wa Afghanistan akaiwakilisha nchi yake katika mkutano wa nchi za Umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi Nato unaotarajiwa kufanyika juma hili.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati mvutano wa kisiasa kati ya wagombea wawili bado unaendelea kuhusu nani anaye mrithi rais Hamid Karzai.

“Afghanistan huenda ikamtuma waziri wake wa ulinzi kuiwakilisha katika mkutano wa Jumuiya ya Kujihami ya Mataifa ya Magharibi Nato, iwapo mvutano wa kisiasa kati ya wagombea wawili kuhusu atakaye chukua urithi wa Hamidi Karzai, utakua haujapatiwa ufumbuzi”, amesema msemaji wa rais Karzai, Aimal Faizi.

Kwa mujibu Faizi, kwa sasa wanaanda kumtuma waziri wa ulinzi kuiwakilisha nchi hiyo katika mkutano wa Nato iwapo jina la rais halitotangazwa kabla ya kufanyika kwa mkutano huo.

Waziri wa ulinzi Bismillah Mohammadi ambaye ni kiongozi wa zamani wa majeshi ya Afghanistan na mshirika wa karibu wa Kamanda Ahmad Shah Massoud aliyeuawa Septemba 9 mwaka 2001.

Mkutano huu wa Nato umepangwa kufanyika Septemba 4 na 5 nchini Uingereza, na utaamuwa kuhusu msaada wa kimataifa kwa serikali ya Afghanistan hususan kuhusu msaada wa polisi na jeshi baada ya kuondoka kikamilifu kwa majeshi ya Nato Desemba 31 mwaka huu.

Hayo yanajiri wakati mvutano wa kisiasa kati ya wagombea wawili bwana Gani na bwana Abdullah ukiendelea kujitokeza. Abdullah hata kama alionekana kushindwa katika duru ya pili ya uchaguzi, ana tumia mbinu za kisiasa ili aweze kushiriki katika serikali ijayo.

Ashraf Ghani (kushoto.), pamoja na Abdullah Abdullah (kulia).
Ashraf Ghani (kushoto.), pamoja na Abdullah Abdullah (kulia). AFP Photo/Wakil KOHSAR

Msemaji wa Ghani, tahir Zaheer ameliambia shirika la habari la Ufaransa kwamba wagombea hao wawili wamekua wakianda aina ya mazungumzo ili kupatia ufumbuzi mvutano huo.