UKRAINE-URUSI-Usalama

Asilimia 70 ya wanajeshi wa Urusi wameondoka Ukraine

Rais wa Ukraine, Petro Porochenko, akibaini kwamba idadi kubwa ya wanajeshi wa Urusi wameondoka katika aridhi ya Ukraine..
Rais wa Ukraine, Petro Porochenko, akibaini kwamba idadi kubwa ya wanajeshi wa Urusi wameondoka katika aridhi ya Ukraine.. REUTERS/Valentyn Ogirenko

Rais wa Ukraine Petro Porochenko amebaini jumatano wiki hii kwamba idadi kubvwa ya wanajeshi wa Urusi wameondoka katika aridhi ya Ukraine siku tano kabla ya utekelezaji wa makubaliano ya kusitishwa mapigano mashariki mwa Ukraine.

Matangazo ya kibiashara

“ Kwa mujibu wa taarifa za mwisho niliyopewa kutoaka kwa idara ya Ujasusi, asilimia 70 ya wanajeshi wa Urusi wameondoka katika aridhi ya Ukraine”, rais Porochenko ametangaza katika kikao cha baraza la mawaziri, kwa mujibu wa mtandao wa tovuti ya ikulu ya Kiev.

Rais porochenko amesema ana imani kuwa mchakato wa amani, ambao umeanza kutekelezwa baada ya makubaliano ya usitishwaji mapigano katika eneo la mashariki kati ya Jeshi na waasi.

“ Hali hii inanifanya kuwa na matumaini ya amani katika siku za usoni” ameongeza rais Porochenko, akiambatanisha yanayojiri sasa mashariki mwa Ukraine na itifaki ya makubaliano ya usitishwaji mapigano yaliyosainiwa ijumaa kati ya serikali ya Kiev na waasi wanaoungwa mkono na Urusi katika jitihada za kusitisha moja kwa moja machafuko.

Machafuko hayo yamesababisha vifo vya watu 2,700.

Mwezi uliyopita Jumuiya ya Kujihami ya Mataifa ya Magharibi Nato,iliitolea wito Urusi kusitisha harakati zake za kijeshi nchini Ukraine, baada ya kuthibitisha kwamba wanajeshi 1000 wamekua wakiendesha harakati za kijeshi nchini Ukraine, huku wengine 20,000 wakiwa waliwekwa kwenye mpaka wa Urusi na Ukraine.