PAKISTANI-TALIBAN

Pakistan: watu waliyoendesha shambulio dhidi ya Malala wakamatwa

Msichana wa kipakistan, Malala Yousafzai, ambaye ni mwanaharakati wa haki za elimu kwa wasichana.
Msichana wa kipakistan, Malala Yousafzai, ambaye ni mwanaharakati wa haki za elimu kwa wasichana. REUTERS/Afolabi Sotunde

Jeshi la Pakistan limetangaza kuwakamata watu waliojaribu kumuua Mala Yousafzai, mwanafunzi msichana mwakla 2012 kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Matangazo ya kibiashara

Malala Yousafzai akiwa na umri wa miaka 15 wakati huo, alishambulia alipokua akitokea shuleni, na kunusurika baada ya kupigwa risase kichwani. Tangu wakati huo Yousafzai amepata umaarufu kimataifa na kuchukuliwa kama mtetezi wa haki kwa elimu ya watoto, hasa wasichana.

Malala Yousafzai mwanaharakati wa haki za elimu kwa wasichana.
Malala Yousafzai mwanaharakati wa haki za elimu kwa wasichana. REUTERS/Gary Cameron

“ Kundi la watu waliloendesha shambulio dhidi ya Malala Yousafzai limekamatwa”, msaemaji wa jeshi, jeneral Asim Bajwa, ametangaza katika mkutano na vyombo vya habari kwenye makao makuu ya jeshi mjini Rawalpindi, karibu na mji kuu wa Pakistan, Islamabad.

Kwa mujibu wa Bajwa, watu hao 10 wamekamatwa wakati wa operesheni ya jeshi ikishirikiana na polisi pamoja na idara ya ujasusi iliyoanzishwa mwezi Juni dhidi ya kundi la Taliban (TTP) pamoja na makundi mengine ya wapiganaji wa kiislam kaskazini magharibi mwa nchi, kwenye mpaka na Afghanistan.

Watu hao ni wapiganaji wa kundi hilo la Taliban (TTP), ambalo lilikiri kuhusika na shambulio hilo dhdi ya Malala Yousafzai, ambaye alikua akitetea haki ya elimu kwa wasichana wa mkoa anakotoka. Amri ya kushambuli amsichana huyo ilitolewa na kiongozi wa kundi hilo la Taliban (TTP), mollah Fazlullah, ameongeza jenerali Bajwa.

Malala Yousafzai alishambuliwa akiwa na wenzake mwaka 2012 wakati walipokua ndani ya basi wakitokea shuleni katika mji wa Mingora, makao makuu ya jimbo la Swat, ambapo wapiganaji wa Taliban walikua walitimuliwa madarakani na jeshi miaka miatau na nusu iliyopita.

Malala alipata umaarufu mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 11, alipoanzisha blogu ya BBC katika lugha ya taifa Ourdou, ambapo alikua akielezea masha duni yaliyokua akiwakabili raia wa jimbo la Swat anakozaliwa.