UKRAINE-URUSI-Mapigano-Usalama

Machafuko mapya yaripotiwa mashariki mwa Ukraine

Mabaki ya basi liliyoshambuliwa kwa roketi Donetsk, jumatano Septemba 1 2014.
Mabaki ya basi liliyoshambuliwa kwa roketi Donetsk, jumatano Septemba 1 2014. REUTERS/Shamil Zhumatov

Mji wa Donetsk unakabiliwa na mashambulizi ya anga yanayoendeshwa na jeshi la Ukraine dhidi ya ngome za waasi. Shule moja limeshambuliwa mapema jumatano wiki hii na kusababisha vifo vya watu 10. Utekelezaji wa mkataba wa Minsk, uliyosainiwa Septemba 5 mwaka 2014, bado unasubiriwa.

Matangazo ya kibiashara

Hakutakuwa na eneo lilopigwa marufuku kwa wanajeshi au waasi mashariki mwa Ukraine kabla ya kuonyeshwa kwa mipaka ya eneo hilo.

Tangu yalipofikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya wanajeshi na waasi wa Ukraine Septemba 5 mwaka 2014, mapigano yamekua yakiendelea na kusababisha vifo vya mamia ya watu ikiwa ni pamoja na raia wengi wa kawaida.

Uwanja wa ndege wa Donetsk pamoja na eneo ndege zinakoegesha vimekua chini ya udhibiti wa jeshi la Ukraine, lakini jeshi la Ukraine lmekua likinyooshea kidole jeshi la Urusi kwamba limekua likiwashambulia.

Kuna uwezekano wanajeshi wa Ukraine wapige kambi kusini mwa mji wa Donetsk, huku uwanja wa ndege wa Donetsk ukichukuliwa na viongozi wa waasi. Hata hivo mkuu wa jimbo la Donetsk, Serhiy taruta amekanusha kwamba mazungumzo kati ya serikali ya Ukraine na waasi yameanza.

Ukosefu wa mazungumzo kati ya serikali na waasi kumesababisha mapigano kutokoma, huku watu zaidi ya 4000 wakiarifiwa kuuawa kutokana na mapigano hayo.