UTURUKI-SYRIA-IRAQ-IS-MAREKANI-Mapigano-Usalama

Muungano wa kimataifa: Dola la Kiislamu laonekana kuwa na nguvu zaidi

Jenerali Allen, mratibu wa muungano wa kijeshi wa kimataifa dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam (katikati), akiwa pamoja na kiongozi wa jumuiya ya mataifa ya kiarabu, Nabil-el-Arabi (kulia), Cairo, nchini Misri, Oktoba 9 mwaka 2014.
Jenerali Allen, mratibu wa muungano wa kijeshi wa kimataifa dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam (katikati), akiwa pamoja na kiongozi wa jumuiya ya mataifa ya kiarabu, Nabil-el-Arabi (kulia), Cairo, nchini Misri, Oktoba 9 mwaka 2014. REUTERS/Asmaa Waguih

Mratibu wa muungano wa kimataifa dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam, jenerali Allen, amethibitisha kuwa wapiganaji hao wameendelea kupiga hatua katika harakati zao.

Matangazo ya kibiashara

Jenerali Allen amezitembelea hivi karibuni nchi zinazoshirikiana na Marekani katika vita dhidi ya Kundi la Dola la Kiislam.

Katika mkutano na waandishi wa habari, afisaa huyo amethibitisha kuwa wapiganaji wa Dola la kiislam wanadhibiti sehemu kubwa nchini Iraq na Syria.

Mratibu huyo wa muungano wa kimataifa dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam, amekiri kuwa wapiganaji wa Dola la Kiislam wamepiga hatua kubwa, huku akisema ni mapema mno kubaini kuwa operesheni inayoendeshwa na Marekani pamoja na washirika wake imefanikiwa kwa kiasi kikubwa

Jenerali Allen amejizuia kusema iwapo kumekuwa na mshindi au mshindwa. Lakini amekiri kwamba katika hatua hii, Iraq imebaki ni tishio kwa Marekani kutokana na wapiganaji wa Dola hilo la Kiislam.

Hata hivo Marekani imesema, jeshi lake limetekeleza mashambulizi kadhaa dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam katika mji wa Kobane na kusababisha mamia ya wapiganaji kuuawa.

Jeshi la Marekani limesema likishirikiana na mataifa mengine , kwa kipindi cha saa 48 zilizopita limetekeleza mashambulizi 40 ya angaa katika mji huo wa Kikurdi.

Rais wa Marekani Barrack Obama amewaambia wakuu wa kijeshi kutoka zaidi ya mataifa 20 yanayoshiriki katika makabiliano ya kuliangamiza kundi hilo kuwa haitakuwa rahisi kuwamaliza wapiganaji hao nchini Syria na Iraq, na ni vita ambavyo vitachukua muda mrefu.