UKRIANE-URUSI-Dilpomasia

Putine na Porochenko wakutana Milan

Rais wa urusi Vladimir Putin na mwenziye wa Ukraine, Petro Porochenko wanapanga kukutana Ijumaa Oktoba 17 mwaka 2014.
Rais wa urusi Vladimir Putin na mwenziye wa Ukraine, Petro Porochenko wanapanga kukutana Ijumaa Oktoba 17 mwaka 2014. REUTERS/Sergei Bondarenko/Kazakh Presidential Office/Pool

Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenziye wa Ukraine Petro Porochenko wanatazamiwa kukutana leo Ijumaa mjini Milan, mkutano ambao utahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo wa kiuchumi na biashara ulianza jana Alhamisi Oktoba 16. Taarifa ya kukutana kwa marais hao wawili imethibitishwa na rais wa Baraza la Italia, Matteo Renzi. Ikulu ya Urusi imefahamisha kwamba viongozi hao wawili wamezungumza kwa sim wiki hii.

Mkutano huo unafanana na mkutano uliyofanyika Juni 6 mwaka 2014 Normandie, mkutano ambao haukuhudhuriwa na rais wa Marekani, Barack Obama. Wakati huo Petro Porochenko alikua ndio bado amechaguliwa, na alikua akijitahidi kutafutia ufumbuzi mgogoro mashariki mwa nchi yake.

Wiki nne baadaye hakuna kilichofanyika, hata kama mkataba wa usitishwaji mapigano ulitiliwa saini Septemba 5 unaendelea kutekelezwa na pande husika katika mgogoro huo.

Hata hivo waasi wa Ukraine wamekua wakijaribu kuweka kwenye himaya yao maeneo waliyopoteza mwezi Julai. Vladimir Putin na Petro Porochenko walikutana kwa mara ya mwisho kabla ya mkataba huo, mkutano ambao haukuzaa matunda yoyote.

Tangu kuafikiwa kwa makubaliano ya usitishwaji mapigano kati ya Ukraine na waasi wa Ukraine, Urusi iliendelea kukabiliwa na vikwazo viliyochukuliwa na mataifa ya Magharibi na Marekani.Ukraine inaandaa uchaguzi utakaofanyika Oktoba 26 wakati ambapo waasi waliojitenga na Ukraine wakijiandalia uchaguzi ambao wanadai utafanyika Novemba 2 mwaka 2014.

Wiki hii rais wa Urusi Vladimir Putine ameagiza wanajeshi wake kuondoka kariu na mpaka.