URUSI-VIKWAZO-UCHUMI-MAENDELEO-UFISADI

Rais Putine ahadi msamaha wa kodi

Katika hotuba yake mbele ya wabunge na Maseneta Alhamisi Desemba 4, rais Vladimir Putin ameahidi msamaha wa kodi kwa wale watakaorejesha mitaji yao nchini Urusi.
Katika hotuba yake mbele ya wabunge na Maseneta Alhamisi Desemba 4, rais Vladimir Putin ameahidi msamaha wa kodi kwa wale watakaorejesha mitaji yao nchini Urusi. dREUTERS/Sergei Karpukhin

Kama kawaida yake ya kila mwisho wa mwaka rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa hotuba mbele ya Wabunge na Maseneta wakiwa pamoja. Putine amechukulia matokeo chanya ya mwaka uliopita na kuonyesha sera zake.

Matangazo ya kibiashara

Sehemu ya kwanza ya hotuba ya rais wa Putin iligubikwa na maelezo kuhusu sera za kigeni za Urusi kabla ya kujihusisha katika uwanja wa kiuchumi.

Rais wa Urusi kwanza amepongeza msimamo wa kitaifa wa kusahihisha na kuonyesha " muungano wa kihistoria kati ya Crimea na Urusi". Putine amebaini kwamba Crimea na Urusi vimekua ni nchi moja, akisema kuwa "Cremea na Urusi ni kama uji na mgonjwa".

Putin hakutaja utatuzi wa mgogoro unaoendelea kusini mashariki ya Ukraine lakini amelani wale wanaounga mkono mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika Kiev, na ukandamizaji dhidi ya wale wanaopinga mauaji. Kwa mujibu wa rais wa Putin, Urusi iko tayari kusaidia kifedha Ukraine ili iweze kujiendeleza, wakati mataifa ya magharibi wanaitumia kwa maslahi yao wenyewe.

" Ukraine ilikuwa kisingizio kuanzisha vikwazo vyenye lengo la kudhoofisha Urusi, ili kukabiliana na kuongezeka kwa uchumi. Lakini Urusi haitokubali itumiwe na mataifa ya magharibi", amesema Putine.

" Uhuru wa Urusi umesalia kuwa sifa muhimu kwa raia na taifa nzima", ameongeza Putine. Putine amebaini kwamba sifa hiyo ni msingi wa uchumi wa Urusi.

Mbali na hilo, kwa mujibu wa rais wa Urusi, vikwazo vina madhara kwa kila mtu, wala si tu kwa yule aliyewekewa vikwazo hivyo.

Putine ameahidi msamaha wa kodi kwa wale ambao watakuwa wamerejesha mitaji yao nchini Urusi. Putine ameahidi pia udhibiti zaidi juu ya tija kwa makampuni makubwa, lakini miaka miwili bila ya ada kwa wale wataanzisha shughuli mbalimbali nchini Urusi, na pia kupambana dhidi ya rushwa huku akiweka mbele mpango wa maendeleo ya majimbo.