Pata taarifa kuu
INDONESIA-Usalama wa Anga

Mabaki ya ndege AirAsia yapatikana

Kwa siku tatu, zoezi la kuitafuta ndege ya shirika la AirAsia ya Indonesia limeendelea katika bahari Java.
Kwa siku tatu, zoezi la kuitafuta ndege ya shirika la AirAsia ya Indonesia limeendelea katika bahari Java. Depuis trois jours, les vols des équipes de recherche se succède
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Mabaki ya ndege ya kampuni ya AirAsia, iliyotoweka Jumapili Desemba 28 ikiwa na abiria 162, yameonekana katika Bahari Java. 

Matangazo ya kibiashara

Mabaki ya ndege hio yameonekana katika eneo la utafutaji, ambalo lina ukubwa sawa na nchi ya Ufaransa.

Msemaji wa jeshi la Indonesia, Agus Dwi Putranto amesema mapema Jumanne asubuhi kuwa timu ya waokoaji walikuwa wameona vitu kumi vikubwa vyenye rangi nyeupe, ambavyo vinafanana na mabaki ya ndege hiyo iliyotoweka.

Wakati huo huo Marekani inaungana na waokoaji wa kimatafa kutoka Australia na Malysia kuitafuta ndege hiyo ambayo inaaminiwa ilianguka baharini lakini hadi sasa hili halijathibitishwa.

Awali watalaam wamesema kuwa wameongeza eneo la kuitafuta ndege hiyo kutoka katika bahari ya Java na sasa utafutaji huo unafanyika pia katika visiwa vya Sumatra na Borneo.

Meli 30 na ndege 15 zinatumika kutafuta mabaki ya ndege hiyo iliyopotea ikitokea mjini Surabaya nchini Indonesia ikielekea nchini Singapore.

Inaelezwa kuwa rubani wa ndege hiyo aliomba kubadilishiwa njia lakini hakupiga tena simu ya dharura kabla ya ndege hiyo kutoweka.

China nayo, imetangaza kutuma meli na ndege yake kusaidia utafutaji wa ndege hiyo huku Australia ikisema inatuma ndege mbili zaidi.

Hii ni ndege ya pili kupotea mwaka huu, baada ya ile ya Malaysia iliyokuwa na abiria 239 kutoweka mwezi Machi ikielekea Beijing nchini China ikitokea Kuala Lumpur na hadi sasa bado haiajapatikana.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.