YEMEN-Mapigano-Usalama

Wanamgambo wa Kishia waivamia Ikulu ya rais

Vizuizi vya kikosi kinachotoa ulinzi wa taasisi za nchi kwenye barabara inayoelekea kwenye Ikulu ya rais katika mji wa Sanaa, Januari 20 mwaka 2015.
Vizuizi vya kikosi kinachotoa ulinzi wa taasisi za nchi kwenye barabara inayoelekea kwenye Ikulu ya rais katika mji wa Sanaa, Januari 20 mwaka 2015. REUTERS/Khaled Abdullah

Kwa mujibu wa afisa wa kijeshi aliyenukuliwa na shirika la habari la Ufaransa AFP, wanamgambo wa Kishia waliokua wameizingira Ikulu ya rais, wameendesha mashambulizi na kwa sasa wanadhibiti boma la rais.

Matangazo ya kibiashara

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya mkutano wa dharura bila hata hivyo kutomriuhusu mtu yeyote asiyekua muhusika kushiriki mkutano huo.

Kulingana na vyanzo viliyonukuliwa na mashirika ya habari Reuters na AFP, wanamgambo wa Kishia waliitdhibiti Ikulu ya rais.

Inaonekana kuwa kikosi kilichokua kinatoa ulinzi wa rais kilindoka katika eneo hilo kabla ya kushambuliwa na wanamgambo hao wa Kishia.

Mapigano yanaendelea karibu na boma la rais wa Yemen, bila hata hivyo kujua hatima ya rais, Abd Rabbo Mansour Hadi. Wakati huohuo, makazi ya Waziri Mkuu bado yanaendelea kuzingirwa na watu wenye silaha wakizuia barabara kuu inazoelekea kwenye makaazi hayo.

Miezi minne baada ya kuingia katika mji mkuu wa Yemen, inaonekana kuwa wanamgambo wa Ansaroullah wameamua kuongeza nguvu dhidi ya utawala uliopo sasa, huku wakiendelea kudhibiti maeneo muhimu ya mji mkuu wa Yemen. Kwa kutaka kutetea hoja yao, wanamgambo wa Kishia wanalani muswada wa Katiba, wakibaini kwamba unawakandamiza raia.

Kulingana na waangalizi wengi, wanamgambo wa Kishia, katika mashambulizi yao mapya wanaufaika na msaada kutoka moja kwa moja kwa wafuasi wa rais wa zamani wa Yemen, Ali Abdullah Saleh, ambaye alitimuliwa madarakani mwaka 2012 baada ya kuongoza Yemen kwa miongo mitatu.