Watu wawili wachunguzwa kuhusika katika mauaji ya Nemtsov
Uchunguzi kuhusu mauaji ya mwanasiasa wa upinzani nchini Urusi, Boris Nemtsov yaliyotokea mwishoni mwa mwezi Februari, umeendeswa kwa kasi masaa 24 yaliyopita.
Imechapishwa:
Jumapili Machi 8 watu wawili wamefunguliwa mashtaka , na mmoja kati ya hao wawili anasadikiwa kukiri kushiriki katika mauaji ya Nemtsov. Washukiwa wengine watatu wamezuiliwa kwa ajili ya uchunguzi.
Watu watano, ambao wote ni wenye asili ya Chechen, wamewekwa kizuizini kwa ajili uchunguzi kuhusu mauaji ya mwanasiasa wa upinzani nchini Urusi Boris Nemtsov, aliye pigwa risasi nne mgongoni alipokua akiondoka katika Ikulu ya Kremlin tarehe 27 Februari mwaka 2015. Wawili kati ya watuhumiwa hao, Zaur Dadaïev na Anzor Goubachev, wamefunguliwa mashtaka Jumapili Machi 8.
Dadaïev alikamatwa Jumamosi Machi 7 katika nchi jirani ya Chechen, na anasadikiwa kuwa alihudumu kwa kipindi cha miaka kumi katika kikosi cha polisi ya Chechen.
Kwa mujibu wa jaji wa Mahakama ya Moscow ya Basmanni, Natalia Mouchnikova, Dadaïev anasadikiwa kukiri kuhusika katika mauaji ya Nemtsov.
Mtuhumiwa wa pili, Anzor Goubachev, kwa upande wake amekana kuhusika katika mauaji hayo. Watuhumiwa wengine watatu ambao walikamatwa mwishoni mwa juma hili katika mji wa Ingouchie wameendelea kutoa taarifa za kuishawishi Mahakama kwamba hawana hatia.
Wachunguzi wanatakiwa kuwa kutoa vithibitisho ndani ya muda wa siku 10 kuhusu kuhusika kwa washukiwa hao katika mauaji ya Nemtsov. Washukiwa hawa wamewekwa kizuizini kwa kipindi cha miezi miwli hadi Aprili 28.