IRAQ-IRAN-IS-Maigano-Usalama

Iraq na Iran zashirikiana kwa kuendesha mashambulizi Tikrit

Gari ya kivita ya jeshi la Iraq pamoja na wanamgambo wa Hashid sha'bi katika vita dhidi ya IS katika kijiji cha Al-Alam, Machi 10 mwaka 2015.
Gari ya kivita ya jeshi la Iraq pamoja na wanamgambo wa Hashid sha'bi katika vita dhidi ya IS katika kijiji cha Al-Alam, Machi 10 mwaka 2015. REUTERS/Thaier Al-Sudani

Tangu mwezi Juni mwaka jana, mji wa Tikrit ulikua chini ya udhibiti wa kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu.  

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Iraq imeapa kuurejesha kwenye himaya yake mji huu. Tikrit mji alikozaliwa aliye kuwa rais wa Iraq Saddam Hussein, umeendelea kushikiliwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu.

Serikali ya Iraq imebaini kwamba kuudhibiti mji wa Tikrit kutaipelekea kuendelea na mapigano hadi katika mji wa Mossoul.

Zaidi ya wanajeshi 20,000 pamoja na wanamgambo wa Kishia wakishirikiana na wapiganaji kutoka jamii ya Wasuni wanaendelea na mapigano dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu tangu siku kumi na tano zilizopita. Lengo ni kudhibiti mji wa Tikrit kabla ya kuendelea na mapigano hadi katika mji wa Mossoul, mji wa pili wa Iraq ambao unashikiliwa pia na wanamgambo wa Islamic State.

Lakini vita vya Tikrit viko mbali na ukweli. Vikosi vya serikali vimekua vikiingia katika vitongoji vya mji wa Tikrit viliyo kaskazini na kusini. Lakini vikosi hivyo vimeapa kupigana hadi kuuteka mji huo wa Tikrit.

Hata hivyo kumekua na taarifa kwamba wapiganaji wa Islamic State wanatumia gesi ya Klorini.
Gesi hiyo huwekwa kwenye silaha za kemikali katika vita nchini Iraq.

Serikali ya Iraq imesema kiasi kidogo cha kemikali kimekuwa kikitumika katika mabomu yanayolenga majeshi yake ambayo yamekuwa yakiwaondoa wapiganaji wa Islamic State katika mji wa Tikrit.