IRAQ-IS-MAPIGANO-USALAMA

Jeshi la Iraq lauzingira mji wa Tikrit

Kwa muda wa zaidi ya siku kumi, Tikrit ni eneo la mapigano kati ya jeshi la Iraq na IS.
Kwa muda wa zaidi ya siku kumi, Tikrit ni eneo la mapigano kati ya jeshi la Iraq na IS. REUTERS/Thaier Al-Sudani

Maelfu ya wanajeshi wa Iraq wamekua wakiuzingira Alhamisi wiki hii mji wa Tikrit, ambo unaendelea kushikiliwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu.

Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao wamekua wakisubiri kuanzisha mashambulizi dhidi ya wanamgambo kadhaa wa Boko Haram ambao wanpiga kambi katika mji huo. Mji wa Tikrit ni muhimu kwa wanajeshi wa Iraq kwa kufanikisha kuudhibiti mji wa Mossoul.

Baada ya siku 11 za mapigano makali, vikosi vya serikali vimechukua uamzi wa kuuzingira mji wa Tikrit. “ Muda huu ni sisi kuuteka mji wa Tikrit”, jeshi la Iraq limeeleza. Uongozi wa jeshi umesema haujataka kuushambulia mji huo. “ Hatuna haja ya kushambulia", jeshi limeongeza.

Jeshi la Iraq limekataa kushambulia kwa haraka mji wa Tikrit kwa kuhofia kupoteza wanajeshi wake na vifaa vya kijeshi. Hata hivyo wanamgambo wa Islamic State waneonekana kujidhatiti katika mji huo.

Awamu ya pili ya vita

Waziri wa ulinzi wa Iraq, Khaled al-Obeidi, amesema wameanza kutumia utaratibu mwengine.

“ Kwa sasa tumeanza kutumia utaratibu mwengine katika plani yetu”, amesema waziri Khaled al-Obeidi, huku akibaini kwamba mji wa Tikrit umezingirwa sehemu zote

Katika vita hivyo, dhidi ya Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu, jeshi la Iraq linashirikiana na makundi mbalimbali ya washia na Wasuni.