CHINA-VYOMBO VYA HABARI-SHERIA-HAKI

China : mwandishi wa habari Gao Yu ahukumiwa kifungo cha miaka saba jela

PEN International imezindua kampeni ya kumuokoa Gao Yu, mwandishi wa habari anayezuiliwa jela Chine.
PEN International imezindua kampeni ya kumuokoa Gao Yu, mwandishi wa habari anayezuiliwa jela Chine. Reuters

Mwandishi wa habari maarufu nchini China Gao Yu amepatikana na hatia ya kuvuja " siri ya nchi" siku ya Ijumaa mjini Beijing.

Matangazo ya kibiashara

Gao Yu amehukumiwa kifungo cha miaka saba gerezani. Adhabu ambayo ni kubwa kwa mwandishi wa habari mwenye umri wa miaka 71. Hukumu hiyo imetangazwa na mahakama, kwenye akaunti yake rasmi ya microblogu na kuthibitishwa na mwanasheria wa mwandishi huyo wa habari.

Kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch, Gao Yu anatuhumiwa kuwa alitumia mtandao wa intaneti unaoendesha kazi yake Marekani hati ya ndani ya Chama tawala cha Kikomunisti, ambacho kilikua kimepania kuimarisha udhibiti dhidi ya mawazo ya kimageuzi.

Hata hivyo mwandishi huyo wa habari amesema atakata rufaa hata kama hana imani ya kuachiliwa huru.

Serikali ya China inamchukulia mpinzani wowote kama tishio kwa sera za chama cha Kikomunisti