IRAN-MAREKANI-UFARANSA-URUSI-CHINA-UJERUMANI-UINGEREZA-NYUKLIA-DIPLOMASIA

Mazungumzo juu ya mpango wa nuklia wa Iran yarejelewa

Wajumbe kutoka mataifa sita yenye nguvu duniani pamoja na Iran yanakutana tena leo Jumatano Aprili 22 mjini Vienna ili kujaribu kupata makubaliano ya mwisho yaliyoafikiwa majuma matatu yaliyopita.

Aprili 2 mwaka 2015, katika mji wa Lausanne, Uswisi, makubaliano ya kisiasa yakifikiwa kati ya Tehran na mataifa yenye nguvu duniani kuhusu suala la mpango wa nyuklia wa Iran.
Aprili 2 mwaka 2015, katika mji wa Lausanne, Uswisi, makubaliano ya kisiasa yakifikiwa kati ya Tehran na mataifa yenye nguvu duniani kuhusu suala la mpango wa nyuklia wa Iran. REUTERS/Ruben Sprich
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo haliyotajwa kuwa ya kihistoria, yatapelekea Iran kuondolewa vikwazo ambavyo vimeisababisha kuporomoka kiuchumi, iwapo itakubali kuachana na kurutubisha madini ya iranium.

Wiki tatu zilizopita, Iran na serikali za Magharibi walisema " vigezo muhimu kwa mfumo wa makubaliano au hatua ", hatimaye zimepigwa.

" Vigezo muhimu kwa mfumo wa makubaliano kuhusu mpango wa Nyuklia wa Iran vimepatikana ", alitangaza mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini, katika mkutano na vyombo vya habari, akiwa pamoja na mwenziye wa Iran katika mji wa Lausanne.

Umoja wa Ulaya na Marekani watasitisha vikwazo vyote vya kiuchumi na kifedha vinavyohusiana na nyuklia. " Tuko mbioni sasa kuandika rasimu ya Nakala ya mpango wa utekelezaji wa pamoja, ikiwa ni pamoja na maelezo ya kiufundi katika wiki na miezi ijayo ", alisema Federica.

Makubaliano ya msingi yanaeleza kwamba theluthi mbili ya uwezo wa sasa wa Iran wakurutubisha uranium usitishwe na kufuatiliwa kwa kipindi cha miaka kumi, kwa mujibu wa chanzo cha Magharibi. Vituo 6000 kwa jumla ya 19000 vinavyorutubisha madini ya uranium vitafuatiliwa.

Hivi karibuni Federica Mogherini alisema kuwa uwezo wa kuipa thamani ya juu uranium kutoka Iran utapunguzwa.