ARMENIA-MAUAJI-USALAM-KUMBUKUMBU

Kumbukumbu ya miaka 100 ya mauaji ya Waarmenia

Waarmenia kutoka Uturuki wamejiunga na wenzi wao duniani kote kusheherekea kumbukumbu ya miaka 100 ya mauaji ya Waarmenia katika vita vya kwanza vya dunia miaka 100 iliyopita.
Waarmenia kutoka Uturuki wamejiunga na wenzi wao duniani kote kusheherekea kumbukumbu ya miaka 100 ya mauaji ya Waarmenia katika vita vya kwanza vya dunia miaka 100 iliyopita. Reuters / O. Orsal

Waarmenia duniani kote wanaadhimisha Ijumaa Aprili 24, miaka mia moja ya mauaji ya watu milioni 1.5 ya mababu zao, yaliyotekelezwa na Waturuki wa mji wa Ottoman wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia.

Matangazo ya kibiashara

Yerevan imeeleza janga hilo kama "mauaji ya kimbari", kauli ambayo imefutiliwa mbali na Uturuki.

Viongozi mbalimbali wakiwemo marais wanahudhuria kumbukumbu hizo, rais wa Ufaransa amewakilishwa na waziri wa ulinzi Yves Le Drian.

Sherehe zinafanyka katika mji mkuu wa Armenia, Yerevan.

Hata hivyo Uturuki inapinga kumbukumbu hizo ikidai kuwa mauaji hayo yalishuhudiwa pia katika makundi mengine zaidi wakati huo wa vita vya kwanza vya dunia na kwamba si Armenia pekee.