NEPAL-TETEMEKO-USALAMA

Tetemeko la ardhi: zaidi ya watu 5,000 wafariki Nepal

Mama huyu raia wa Nepal akiwa kwenye magofu ya nyumba yake, iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi la Aprili 25 mwaka 2015.
Mama huyu raia wa Nepal akiwa kwenye magofu ya nyumba yake, iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi la Aprili 25 mwaka 2015. REUTERS/IFRC/Palani Mohan

Nchini Nepal, idadi ya watu walipoteza maisha kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Jumamosi mwishoni mwa juma lililopita imeendelea kuongezeka siku baada ya siku. 

Matangazo ya kibiashara

Mpaka sasa inaaminika kuwa watu 5057 wamepoteza maisha kufuatia tetemeko hilo la ardhi, huku wengine takriban 8,000 wakijeruhiwa.

Hata hivyo serikali ya Nepal imeendelea kunyooshewa kidole cha lawama kwamba haijafanya chochote.

Awali wizara ya mambo ya ndani imetoa takwimu ya watu 4,300 ambao wamepoteza maisha kufuatia tetemeko hilo la ardhi, huku akiongeza kuwa watu wengine 7,953 wamejeruhiwa.

Watu zaidi ya mia moja wanaripotiwa kupoteza maisha katika mataifa jirani kama China na Baghladesh.

Wakati huo huo, wanajeshi tisa kati ya kumi nchini Nepal wanahusika na shughuli za uoakozi wakati huu nchi hiyo ikiendelea kuomba msaada wa kibinadamu kutoka kwa Jumuiya ya Kimataifa.

Tayari China, India, Marekani na Uingereza zimetuma misaada ya kibinadamu kuwasaidia maelfu ya walioathiriwa.

Kwa sasa Nepal inahitaji chakula, blanketi, helikopta, madaktari na hata madereva .

Waki wa tetemeko hilo la ardhi kulikuwa na wakwea milima 200 ambao walikuwa katika mlima wa Everest na juhudi za kuwaokoa zinanendelea kwa sasa.

Mji Mkuu wa Kathmandu ndio uliathiriwa zaidi na tetemeko hilo la ardhi baya zaidi ndani ya miaka 80.