INDONESIA-SHERIA-MAUAJI

Indonesia: watu 8 waliohukumiwa adhabu ya kifo wauawa

Nchini Indonesia, watu wanane waliohukumiwa adhabu ya kifo kwa kosa la biashara ya madawa ya kulevya wameuawa Jumanne usiku wiki hii kwa kupigwa risasi.

Makati, Ufilipino, maandamano ya kuunga mkono Mary Jane Veloso ambaye ameponea kuuawa baada ya adhabu yake kuahirishwa Jumanne Aprili 28 mwaka 2015.
Makati, Ufilipino, maandamano ya kuunga mkono Mary Jane Veloso ambaye ameponea kuuawa baada ya adhabu yake kuahirishwa Jumanne Aprili 28 mwaka 2015. REUTERS/Erik De Castro
Matangazo ya kibiashara

Raia saba wa kigeni ikiwa ni pamoja na raia wawili kutoka Austalia, raia mmoja wa Brazil, raia watatu wa Nigeria na raia mmoja wa Gabon ni miongoni mwa waliouawa. Raia mmoja kutoka Ufilipino ambaye ni miongoni mwa waliohukumiwa adhabu ya kifo amenusurika na adhabu hiyo katika dakika za mwisho.

Kama walivyotangaza, viongozi wa Indonesia wametekeleza adhabu hiyo ya kifo usiku wa manane Jumanne wiki hii. Raia hao ikiwa ni pamoja na raia wawili wa Australia, raia mmoja wa Brazil, raia watatu wa Nigeria, raia mmoja wa Ghana na raia mmoja wa Indonesia wameuawa kwa kupigwa risasi katika jela la kisiwa kiliyo mbali cha Nusakambangan.

Pamoja na shinikizo mbalimbali za kimataifa na maombi kutoka kwa ndugu na jamaa za watu hao waliokua wamehukumiwa adhabu ya kifo kwa ajili ya msamaha, Jakarta ilibakia na msimamo wake mpaka mwisho. Rais Joko Widodo, ambaye aliingia madarakani katika majira ya joto kufuatia sehemu ya kampeni yake ya kupambana na madawa ya kulevya, ambapo alisema kutowasamehe watu watanojihusisha na madawa hayo ya kulevya. Utekelezaji wa adhabu kwa watu hao waliohukumiwa ulikuwa unatarajiwa.

Katika dakika za mwisho, mmoja kati ya watu hao waliohukumiwa kifo, mwanamke ambaye ni raia wa Ufilipino amenusurika kuuawa, jambo ambalo limewashangaza wengi. Rais Joko Widodo ameahirisha utekelezaji wa adhabu ya kifo kwa raia huyo wa Ufilipino baada ya kujisalimishana kudai kuwa alikua akijihusisha na biashara ya binadamu. Lakini uamzi huo wa kuahirisha utekelezaji wa adhabu hiyo ni wa muda mfupi kwa raia huyo wa Ufilipino pamoja na Serge Atlaoui, raia wa Ufaransa, ambaye aliondolewa katika dakika za mwisho kwenye orodha ya watu ambao walikua wanatarajiwa kuuawa.

Waziri mkuu wa Australia Tony Abbot amelaani mauaji hayo na kuyaita ya kinyama na amemwambia balozi wake nchini Indonesia kurudi nyumbani.

Brazil pia imelaani hatua ya kuawa kwa raia wake mmoja, huku
Mataifa ya Magharibi pamoja na Mashirika ya kutetea haki za binadamu duniani yamekuwa yakitoa wito kwa Indonesia kutotekeleza hatua hiyo bila mafanikio.
Indonesia imetetea uamuzi wake na kusema inapambana na vita dhidi ya dawa za kulevya nchini humo.