UN-NEPAL-MSAADA-HAKI

UN yawataka wafadhili kuisaidia Nepal

Msaada aa kibinadamu kwa Nepal ukiwasili katika uwanja wa ndege wa Bangkok Aprili 28 mwaka 2015.
Msaada aa kibinadamu kwa Nepal ukiwasili katika uwanja wa ndege wa Bangkok Aprili 28 mwaka 2015. REUTERS/Chaiwat Subprasom

Umoja wa Mataifa unaomba msaada wa kifedha wa Dola Milioni 415 kutoka kwa wafadhili ili kuwasaida maelfu ya watu waliathiriwa na tetemeko la ardhi nchini Nepal.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa unasema fedha hizo zitasaidia serikali kutoa misaada ya kibinadamu kama makaazi kwa waathiriwa kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo.

Wakaazi wa mji Mkuu Kathmandu waliathiriwa na tetemeko hilo wanasema wamesahaulika na hakuna usaidizi wowote wanaopata kutoka kwa serikali.

Wakaazi hao wamekabiliana na polisi wakati wakijaribu kuondoka katika mji huo mkuu kwa kwenda kutafuta msaada maeneo mengine.

Serikali ya Nepal inasema imeelemewa kutoa usaidizi wowote wa kibinadamu na inawategemea wasamaria wema kutoka Mataifa ya kigeni.

Wakati hayo yakijiri maofisa wanaoshughulikia mkasa huu wanasema idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na tetemeko hilo la ardhi imefikia 5,500.