CHINA-MDORORO WA UCHUMI-MASOKO YA HISA

Soko la Hisa la Shanghai laanza kupata nafuu

Ubao unaoonesha jinsi sarafu ya China inavyouzwa kwa siku ya leo alhamisi Agosti 27 mwaka 2015.
Ubao unaoonesha jinsi sarafu ya China inavyouzwa kwa siku ya leo alhamisi Agosti 27 mwaka 2015. AFP/AFP

Soko la Hisa la Shanghai limepata nafuu ya kupanda kwa kiwango cha 3% juu ya Soko la hisa la Hong kong. Hali hii imeshuhudiwa mapema Alhamisi wiki hii, baada ya hatua kadhaa kuchukuliwa, hususan kushuka kwa viwango vya riba, uamzi ambao umechukuliwa na benki kuu ya China baada ya siku mbili ya mdororo wa kifedha tangu Jumatatu Agosti 24.

Matangazo ya kibiashara

Katika biashara za kwanza, sarafu ya Shangai imekua imepanda 1.73%, au pointi 50.74 kwa pointi 2978.03. Jumatano wiki hii ilikuwa imepoteza 1.27%.

Soko la Hisa la Shenzhen lilikua limepanda kutoka 1.64% pointi 1723.54.

Katika biashara ya awali, sarafu ya China imekua ikifaidika pointi 15. 82 kwa pointi 2980.79. Kwa upande wake.

Kwa upande wake, Sarafu ya Hang Seng katika mji wa Hong Kong imepanda kwa 3.22% kwa pointi 21,758.62, baada ya siku moja kabla ikiwa katika hasi (-1.52%).

" Hofu kwenye soko imeongezeka ", Zhang Yanbing, mchambuzi katika shirika la Zheshang Securities ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

Katika mji wa Tokyo, Soko la Hisa liliongezeka kwa kiwango kidogo Jumatano wiki hii katikati ya kikao baada ya vikao sita ambavyo viliishia patupu, baada ya kusaidiwa na masoko ya Ulaya Jumanne wiki hii.

Katika jitihada mpya ili kusaidia uchumi usiendelei kuporomoka na kuwahakikishia wawekezaji, benki kuu ya China (PBOC) ilitangaza Jumanne wiki hii kushuka kwa viwango vya riba.

Tangu Jumatano, kiwango cha mikopo kwa mwaka na kiwango cha amana kwa mwaka vimepunguzwa kwa pointi 25 na kufikia 4.60% (kwa mikopo) na 1.75% (kwa amana).