MALAYSIA-UCHUNGUZI-AJALI

Ajali ya MH17: wachunguzi watoa ripoti yao ya mwisho

Miezi kumi na tano baada ya ajali ya ndege MH17 ya shirika la ndege la Malaysia Airlines mashariki mwa Ukraine na kusababisha vifo vya watu 296, wachunguzi kutoka Uholanzi wanatazamia kutoa ripoti yao ya mwisho Jumanne hii, ripoti ambayo inaweza kusababisha mvutano kati ya nchi za Magharibi na Moscow.

Shada za maua zikiwekwa kwenye mabaki ya MH17, ndege ya Malaysia Airlines, Julai 26, 2014, Grabove katika jimbo la Donetsk, Ukraine.
Shada za maua zikiwekwa kwenye mabaki ya MH17, ndege ya Malaysia Airlines, Julai 26, 2014, Grabove katika jimbo la Donetsk, Ukraine. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Wakati ambapo Ofisi ya Usalama ya Uholanzi (OVV) imekua ikihitimisha maandalizi yake kwa ajili ya kutoa ripoti yake ambayo inasubiriwa kwa hamu na gamu, Urusi tayari imehiandaa kwa majibu baada ya kukanusha vikali kuhusika kwa njia yoyote katika tukio la Julai 17 mwaka 2014.

Ofisi ya Usalama ya Uholanzi, ambayo inaendesha uchunguzi tangu Boeing 777 ya Malaysia Airlines kutoweka kwa rada, inatazamia kuwasilisha ripoti yake ya mwisho saa 7:15 mchana (sawa na 5:15 mchana saa za kimataifa) katika kambi ya jeshi la anga la Gilze-Rijen, kusini mwa Uholanzi.

Watu wote 298 waliokua katika ndege hiyo, ikiwa ni pamoja na theluthi mbili ya raia wa Uholanzi, walipoteza maisha wakati ndege ilipodunguliwa katika anga la eneo linakabiliwa na mapigano kati ya waasi wanaoungwa mkono na Urusi na vikosi vya serikali vya Ukraine, wakati ambapo ndege hiyo ilikua ikisafiri kutoka Amsterdam kwenda Kuala Lumpur.

Ukraine na Marekani waanadai kwamba ndege hiyo ilidunguliwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi kwa kombora aina ya BUK lililotengenezwa na Urusi. Wachambuzi wanasema waasi wanaoungwa mkono Urusi walidungua Boeing 777 "kwa makosa", wakifikiri kwamba waliilenga ndege ya kijeshi ya Ukraine.