Pata taarifa kuu
MALAYSIA-UCHUNGUZI-AJALI

Ukraine: ndege MH17 ilidunguliwa kwa kombora la Urusi aina ya BUK

Mkurugenzi wa Ofisi ya Uchunguzi wa usalama (OVV), Tjibbe Joustra, katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya uchunguzi katika ajali ya ndege ya shirika la Malaysia Airlines (MH17) nchini Ukraine mwezi Julai 2014.
Mkurugenzi wa Ofisi ya Uchunguzi wa usalama (OVV), Tjibbe Joustra, katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya uchunguzi katika ajali ya ndege ya shirika la Malaysia Airlines (MH17) nchini Ukraine mwezi Julai 2014. REUTERS/Michael Kooren
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Ndege ya Malaysia Airlines ambayo ililipuka katika anga ya Ukraine Julai 17, 2014, na kuwaua watu 298, ilidunguliwa kwa kombora aina ya BUK lililorushwa kutoka eneo la mashariki mwa Ukriane linalodhibitiwa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Haya ni matokeo ya utafiti wa kimataifa uliofanywa na Uholanzi na ambapo ripoti imetolewa Jumanne hii, Oktoba 13. Lakini matokeo hayo yamepingwa na Urusi, ambayo inatumia uwezo mkubwa ili kuwashawishi kwamba Ukraine ndio ilihusika na ajali hiyo.

Ripoti inasema kuwa kombora lilirushwa kutoka mashariki mwa Ukraine. Hata hivyo, haisemi chanzo watu waliohusika na ajali hiyo. Dakika chache kabla ya kutolewa kwa ripoti ya wachunguzi wa Uholanzi, Waziri Mkuu Ukraine amesema alikuwa aliamini baada ya ajali hiyo kuwa ndegeilidunguliwa navikosi maalum vya Urusi.

" Kwa maoni yetu, kombora lilirushwa kutoka eneo linalodhibitiwa na wapiganaji wa Urusi na hakuna shaka kwamba waasi wanaoungwa mkono na Urusi waliokua wamelewa walikua na uwezo wa kurusha kombora la aina ya BUK. Hii ina maana kwamba ni askari wataalamu wa Urusi ambao waliendesha shambulio hilo ", Arseniy Yatsenyuk amesema Jumanne wiki hii katika mkutano wa serikali.

Katika ripoti yao, wachunguzi kutoka Uholanzi wamebaini kwamba ndege ya shirika la Malaysia Airlines ilidunguliwa baada ya sehemu ya mbele ya ndege hiyo kulipuka. Wataalam na maafisa wa serikali kutoka nchi za Magharibi wanaamini kuwa ndege hiyo ililidunguliwa, labda bila kukusudia, na waasi ambao waliifananisha na ndege ya jeshi la Ukraine.

Wakati huo huo Urusi imekanusha tuhuma hizo dhidi yake na kuinyooshea kidole Ukraine kwamba ndio ilihusika na udunguaji wa ndege ya shirika la ndege la Malaysia Airlines.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.