AFGHANISTAN-PAKISTAN- INDIA-TETEMEKO-USALAMA

Tetemeko kubwa la ardhi latikisa eneo la kusini mwa Asia, zaidi ya watu 200 wafariki

Tetemeko kubwa la ardhi lenye nguvu ya 7.5 kwenye vipimo vya Richter, limetikisa Jumatau wiki hii eneo la kusini mwa Asia, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 180 nchini Pakistan na Afghanistan, ikiwa ni pamoja na wanafunzi 12 wa Afghanistan waliofariki kwa kukanyagana wakati wa kukimbia wakiondoka katika madara ya shule.

Wapakistan kukusanyika karibu na vifusi vya nyumba nyingi, baada ya tetemeko kubwa la ardhi katika eneo la Bajaur, Pakistan, Oktoba 26, 2015.
Wapakistan kukusanyika karibu na vifusi vya nyumba nyingi, baada ya tetemeko kubwa la ardhi katika eneo la Bajaur, Pakistan, Oktoba 26, 2015. ANWARULLAH KHAN/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya watu wengine wamejeruhiwa na tetemeko hilo, lililodumu muda mrefu, na hivyo kusababisha maelfu ya watu kuondoka mitaani nchini India, Afghanistan, Pakistan na Tajikistan.

Kulingana na Taasisi ya Marekani ya Jiolojia (USGS), uti wa tetemeko hilo unapatikana katika eneo la Jurm, katika milima ya mbali ya Badakhshan, Kaskazini Mashariki mwa Afghanistan. kwenye kina cha kilomita 213.5.

Nchini Afghanistan, watu waliopoteza maisha ni 33, ikiwa ni pamoja na tisa kutoka Badakhshan, kumi kutoka Nangarhar (mashariki), na wawili kutoka jimbo la Baghlan pamoja na wanafunzi kumi na mbili. Kuna uwezekano idadi hii iongezeke, viongozi wameonya.

Idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha imeshuhudiwa katika nchi jirani ya Pakistan, ambapo takriban watu 150 wamepoteza maisha, kulingana na takwimu ziliyotolewa na serikali za mitaa na mikoa.

Jeshi limethibitisha vifo vya watu 123 na kubaini kwamba zaidi ya watu 950 wamejeruhiwa. Katika mji mkuu Islamabad, baadhi ya majengo yamepasuka.

Miaka kumi iliyopita nchini Pakistan, Oktoba 8, 2005, tetemeko leny ukubwa wa 7.6 ambapo kitovu chake kilipatikana kwenye umbali wa zaidi ya kilomita mia moja ya kile cha leo Jumatatu tetemeko hilo liliwaua zaidi ya watu 75,000. Lakini uti wake ulikua mfupi, na mtikisiko wake ulisababisha uharibifu mkubwa.