AFGHANISTAN-PAKISTAN-USALAMA

Kambi ya jeshi la India yashambuliwa karibu na Pakistan

Askari polisi akipiga doria karibu na kambi ya jeshi la anga la India katika eneo la Pathankot katika jimbo la Punjab, karibu na mpaka wa Pakistan: kambi hiyo imeshambuliwa Jumamosi hii, Januari 2, 2016.
Askari polisi akipiga doria karibu na kambi ya jeshi la anga la India katika eneo la Pathankot katika jimbo la Punjab, karibu na mpaka wa Pakistan: kambi hiyo imeshambuliwa Jumamosi hii, Januari 2, 2016. © REUTERS/ANI

Kundi la watu wanne au watano wenye silaha wameshambulia mapema Jumamosi hii, Januari 02 kwenye saa 9:30 Alfajiri saa za India kambi ya jeshi ya India, karibu na mpaka na Pakistan.

Matangazo ya kibiashara

"Tunaamini kwamba wawili wa washambuliaji wameuawa, wakati wengine wakiaminika kuwa wamekimbilia katika moja ya majengo", mkurugenzi mkuu wa polisi ya wilaya ya Pathankot katika jimbo la Punjab (kaskazini magharibi mwa India ) amesema. Kwa mujibu wa askari polisi mmoja, hakuna ndege hata moja ya jeshi katika kambi hiyo iliyoweza kuharibiwa.

Vikosi vya usalama vimeendelea kutafuta kujua watu waliohusika na shambulio hilo. Afisa mwandamizi wa usalama mwenye cheo cha juu ambaye hakutaka kutaja jina lake ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba wanaoshukua kuwa waliohusika na shambulio hilo ni wapiganaji wa kundi la kiislamu la Jaish-e-Muhammad, lililoundwa mwaka 2000 na Idara ya Ujasusi ya kijeshi ya Pakistan (ISI ) ili kuongeza shinikizo kwa India kuhusu jimbo la Kashmir. Huenda ikawa washambuliaji wa kujitoa mhanga ambao wamewatapeli walinda usalama katika kambi hiyo kwa kuvaa sare za kijeshi.

Serikali ya India ilikua ilitangaza hali ya tahadhari katika jimbo la Punjab Ijumaa hii baada ya wizi wa gari iliyokua ikiendeshwa na afisa mwandamizi wa polisi, gari ambalo inasadikiwa kuwa lilibwa na watu watano wenye silaha ambao walikua walivalia sare za kijeshi. Gari hilo baadaye lilikutwa limetelekezwa kwenye barabara inayoelekea Pathankot-Jammu, barabara kuu inayounganisha jimbo linalokabiliwa na vurugu la Kashmir kwenye tambarare ya India.

Mahusiano kati ya New Delhi na Islamabad yaendelea kudorora

Tangu nchi hizi mbili kupata uhuru kutoka mikononi mwa Uingereza mwaka 1947, India na Pakistan zimeanzisha vita kuhusu udhibiti wa moja kwa moja wa jimbo la Kashmir, katika mlima wa Himaya ambapo kila nchi inadhibiti sehemu moja, huku nchi zote mbili zikitaka udhibiti wa eneo lote la jimbo hilo. New Delhi inalishtumu mara kwa mara jeshi la Pakistan kurusha risasi na makombora katika jimbo la Punjab kwa kisingizio cha waasi wanaopenya na kuingia kwenye mpaka, na baadaye kuendesha mashambulizi dhidi ya polisi ya jimbo Punjab.